• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

JAFO AZINDUA WIKI YA MAZINGIRA

Imetumwa : June 1st, 2023



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amezindua wiki ya maadhimisho ya Mazingira Duniani yanayoanza kuadhimishwa tarehe 01/06/2023 hadi tarehe 05/06/2023 siku ya kilele Duniani kote.

Uzinduzi huo umefanyika mapema hii leo 01/06/2023 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege ambapo awali zoezi la usafi wa barabara na mitaro ya maji ya mvua umefanyika kuanzia katika Barabara ya NAM hotel hadi katika viwanja vya Shule hiyo ambapo Mhe. Dkt. Jafo na Mhe. Senyamule Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na wadau mbalimbali wa mazingira walipata fursa ya kupanda miti shuleni hapo.

"Mkoa wa Dodoma umepewa nafasi ya kipekee ya kupanda miti millioni 40 ukilinganisha na Mikoa Mingine, Zoezi la siku ya Mazingira Duniani ilianzia nchini Sweden baada ya kuona uharibifu wa mazingira unaendelea kwahiyo ilitengwa siku maalum ili kuwakumbusha watu kutunza na kuyahifadhi Mazingira.

"Sherehe za Mazingira za Mwaka huu zinafanyika kitofauti kwasababu hatuna mpango wa kuadhimisha siku ya Mazingira ukumbini, Ila tutafanya kwa vitendo kwa kufanya usafi na kupanda miti katika mitaa mbalimbali ya Nchi yetu na siku ya kilele makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango atafanya Usafi na wanaDodoma katika maeneo ya Makulu hadi Chimwaga kilipo chuo Kikuu cha Dodoma", Amesisitiza Dkt. Jafo

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa kuendelea kushirikiana vizuri na Ofisi ya Mkoa huo katika kutekeleza azma ya Serikali ya kukijanisha Dodoma

"Kipekee niwashukuru Ofisi ya Makamu wa Rais tumekuwa tukisema mara nyingi Dodoma imekuwa ikipewa kipaumbele katika sekta mbalimbali lakini nguvu kubwa imewekwa pia katika utunzaji wa mazingira tangu Mhe.Rais Samia alipokuwa Makamu wa Rais alilifanya zoezi hili kwa ukubwa tunamshukuru sana kwasababu hata wasaidizi wake mmekuwa mstari wa mbele kulitekeleza hili.

"Mlitoa maelekezo ya kupanda miti katika vyanzo vya maji na tumefanya hivyo katika bonde la Mzakwe na miti Ile inaendelea vizuri pia katika kuendeleza kampeni ya soma na mti na tumekwisha fanikiwa kupanda miti katika Shule zote za Msingi na Sekondari za Mkoa wetu. Katika kipengele cha kuzuia mifuko ya plastiki tumekuwa tukishiirikiana na NEMC na hadi sasa tumefanikiwa kuiondoa sokoni na tunashirikiana vizuri na Mikoa jirani katika kulitekeza Jambo hilo", Amesema Senyamule

Kilele cha siku ya Mazingira Duniani kinatarajiwa kufanyika Juni 5 mwaka huu ambapo kitaifa yataadhimishwa katika Jiji la Dodoma na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Phillip Mpango huku yakiwa na kaulimbiu ya "Pinga Uchafuzi wa Mazingira Unaotokana na Taka za Plastiki" na maadhimisho ya siku hiyo Kidunia yanatarajiwa kufanyika nchini Ivory coast.



Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.