• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

Imetumwa : August 21st, 2025

Na. Elizabeth S. Dai & Bilali Juma

Habari- DODOMA Rs

Wananchi na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma wameaswa kuendelea kuchagiza Utalii wa Mkoa huo kwa maslahi ya kuchangia uchumi wa Taifa na Mkoa kupitia watalii watakaotembelea vivutio vya kitalii vinavyopatikana katika mazingira yao.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo, aliyemuwakilisha Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, katika hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa kukuza Utalii wa Mkoa wa  Dodoma iliyofanyika Agosti 21, 2025, kwenye ukumbi wa Mabele Jijiji Dodoma.

“Wananchi wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na sisi wenyewe ni kuhakikisha tunachagiza katika upande wa utalii. Bahati nzuri tuna sifa ya ukarimu, ukitaka watu wakarimu njoo Dodoma utawakuta, hivyo tutumie ukarimu wetu kuhakikisha ajenda hii ya utalii inasonga mbele kwa maslahi mapana ya Tanzania na halikadhalika Mkoa wetu wa Dodoma”.

Aidha Dkt. Jafo amewakaribisha wadau wa utalii kushirikiana na Serikali ya  Mkoa, “Wadau wa maendeleo wahakikishe kwamba tunachagiza ajenda hii kwa pamoja , tunawakaribisha Dodoma ili wafanye kazi kwa3 kushirikiana na serikali kuu lengo kubwa ni kwamba ajenda hii ya kuhakikisha Dodoma inakua kitovu cha Utalii lazima tuifanye kwa pamoja”, amewakaribisha Dkt. Jafo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameweka bayana namna mkakati huo utakavyokua chachu ya kuchochea Utalii,  na  chanzo cha kuongeza pato la wananchi  na Mkoa kwa ujumla.

“Leo hii tunayo furaha kubwa kuona mawazo yalianza kama ndoto na baadae kwenye utekelezaji lakini leo  tunayo ‘document’ ambayo sasa inatuongoza kila tunapotaka kufanya utalii kuwa ni kipaumbele cha pili cha uchumi wa mkoa, tunatakiwa tufanye nini, tupite wapi na tutafika wapi kwa namna gani, kwahiyo sisi leo tunajiona ni watu wenye furaha sana kuwa na siku hii ya pekee ya uzinduzi wa kitabu hiki.

‘’Pamoja na jitihada hizi  sekta binafsi pia zimechangia kwa kiasi fulani katika kukuza uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Dodoma, ujenzi wa mahoteli , ‘apartments’ ambazo zinavutia watu kuja kukaa Dodoma na wakija hawapati shida. pia makampuni ya utalii yameanzishwa yote hayo yanapatikana Dodoma lakini uwekezaji huu ni matokeo ya mazingira wezeshi yaliyowekwa na serikali ili kurahisisha uwekezaji”, amebainisha Mhe. Senyamule

Hatahivyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya maliasili na Utalii Bw. Nkoba Mabula ameupongeza Mkoa wa Dodoma kwa kuanzisha mkakati huo na kuitaka Mikoa mingine kuiga ili kukuza uchumi wa nchi kupitia Sekta ya Utalii nchini.

Hafla hiyo imeambatana na uzinduzi wa kitabu cha “Mkakati wa Kukuza na Kuendeleza Utalii Dodoma 2025” pamoja na kuonyesha tamaduni mbalimbali za makabila yanayopatikana Dodoma yakiongozwa na kabila la Wagogo.


#dodomafahariyawatanzania.

#wekezadodomastawishadodoma.

#keroyakowajibuwangu.

#mtiwangubirthdayyangu.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.