• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

Imetumwa : August 19th, 2025

Na. Bilali A. Juma

Habari – DODOMA RS

Mashirika ya misaada ya kibinadamu Duniani yameshauriwa kuweka mfumo endelevu wa utoaji huduma kwa kujenga ustahimilivu wa kukabiliana na majanga mbalimbali yanayojikeza.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi, aliyemuwakilisha Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, katika maadhimisho ya Siku ya Watoa Misaada ya Kibinadamu Duniani yaliyofanyika Agosti 19, 2025, kwenye Ukumbi wa Mabele Jijini Dodoma.

" Katika kukabiliana na majanga mbalimbali Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, mashirika ya misaada ya kibinadamu, taasisi na mashirika yasiyo ya Kiserikali huratibu juhudi mbalimbali za kuokoa maisha na mali za wananchi.  Hatua hizo huhusisha utoaji wa chakula na malazi ya muda, huduma za afya pamoja na msaada wa kisaikolojia na kijamii".

Aidha Mhe. Lukuvi  amebainisha hatua za haraka zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha inarudisha mazingira yaliyoathirika katika hali yake ya awali.

"Serikali huchukua jitihada za haraka za kurudisha miundombinu iliyoharibiwa ili kuwawezesha wananchi kurejea katika hali ya kawaida mapema iwezekanavyo, uzoefu huo umethibitisha umuhimu wa kuwa na mifumo thabiti ya ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na jamii kwa ujumla.

Vile vile umeonyesha haja ya kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema na kujenga uwezo wa jamii kustahimili madhara kabla majanga hayajatokea, " amesema Mhe. Lukuvi

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, aliwataka wadau kushirikiana kwa karibu zaidi katika kukabiliana na majanga, akibainisha kuwa mshikamano ni msingi wa usalama wa wananchi.

Naye  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary S. Senyamule, alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kudumisha amani na utulivu Nchini, hali inayowawezesha wananchi kufanya kazi kwa usalama na utulivu.

Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu: “Kuimarisha utoaji wa huduma za kibinadamu na ustahimilivu dhidi ya majanga” yameandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na DINGONET, ambapo yalisisitiza pia  umuhimu wa amani na mshikamano Duniani.

Maadhimisho hayo huadhimishwa kila Agosti 19 ikiwa ni kumbukizi ya wafanyakazi 22 wa misaada ya kibinadamu, waliofariki kwa mlipuko wa  bomu uliotokea katika hoteli ya Canal huko Baghdad, Iraq.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.