• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

JAMII YAPIGWA MARUFUKU KUTUMIA WATU WENYE ULEMAVU KAMA KITEGA UCHUMI

Imetumwa : December 6th, 2024

Na; Happiness E. Chindiye

Habari - Bahi DC

Katibu tawala Wilaya ya Bahi Bi. Sara Ngalingasa amepiga marufuku baadhi ya watu ambao wanawatumia Watu Wenye Ulemavu kuwa sehemu ya kujipatia kipato kwa kuwazungusha mitaani kufanya kazi ya kuomba omba.

Bi.Ngalingasi  ametoa kauli hiyo leo Disemba 06,2024 wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  kwenye  maadhimisho ya Kimkoa ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu yaliyotanguliwa na kongamano lililojumuisha washiriki  kutoka Muungano wa Vyama vya Watu Wenye Ulemavu SHIVIWATA yaliyofanyika Wilayani  Bahi.

"Jamii inatakiwa kutambua wazi kuwa ulemavu siyo kuwa masikini au kuondolewa utu wa mtu bali Mtu Mwenye Ulemavu anatakiwa kuthaminiwa na kupewa haki yake kama alivyo mtu mwingine.

Tumeshuhudia baadhi ya wazazi au walezi wakiwatumia watoto wenye ulemavu vibaya badala ya kuwapatia haki yao ya msingi kama vile kuwapeleka shule, wao wamekuwa wakiwatumia vibaya kwa kuwazungusha mitaani  kuombaomba jambo ambalo si sahihi kulifanya.

Lazima tutambue kuwa watu wote wenye ulemavu wanatakiwa kupata haki zao za msingi na ulemavu siyo tiketi kuwa mnyonge au kunyanyapaliwa au kujinyanyapaa"ameeleza Ngalingasi.

Kwa upande wa uongozi wa SHIVIWATA Mkoa wa Dodoma wameishukuru Serikali ya Mkoa huu kwa kuendelea kuwatambua Watu Wenye Ulemavu na kuwapa kipaumbele katika kuwapatia huduma.

“Tunaishukuru Serikali ya Mkoa wetu wa Dodoma imeendelea kuwatambua Watu Wenye Ulemavu na kuwapatia huduma

mbalimbali ikiwa ni pamoja na msaada wa kisaikolojia na kijamii, vifaa saidizi

kama vile fimbo nyeupe, miwani kwa wenye uoni hafifu, viti mwendo, baiskeli za magurudumu matatu na magongo ili kuwawezesha kumudu mazingira yao.

Mchanganuo wa huduma zilizotolewa na idadi ya vifaa ndani ya Mwaka huu ni Miwani 109, fimbo nyeupe 70, miamvuli 84, mafuta maalum ya kukinga mionzi ya jua 857, kofia za kukinga na jua 196, baiskeli za magurudumu matatu 32.

“Watu wenye ulemavu 2,061 walipatiwa huduma ya msaada wa kisaikolojia na kijamii na 1,693 walipatiwa huduma za matibabu kwa msamaha. kwa mwaka 2024/2025 Halmashauri 5 zilitenga kiasi cha sh. 19,090,000/- kwa ajili ya huduma kwa Watu Wenye Ulemavu.”- wameeleza Viongozi wa SHIVYAWATA

 Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Kukuza Uongozi wa Watu Wenye Ulemavu kwa Ajili ya Mustakabali

Jumuishi na Endelevu”.


&&&


#mtiwangubirthdayyangu

#dodomafahariyawatanzania

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.