• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KIWANDA CHA MVINYO KUFUFUA MATUMAINI YA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA

Imetumwa : October 8th, 2025

Na. Sizah Kangalawe

Habari- Dodoma Rs

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amepongeza Jiji la Dodoma kwa ubunifu katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu uendelezaji wa  zao la zabibu na uzalishaji wa mvinyo Jijini humo.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika eneo la Hombolo kilipo kiwanda cha zabibu kinachomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mhe. Senyamule alisema

"Leo ninayo furaha kubwa na nimpongeze Mkurugenzi wa Jiji na wilaya yote ya Dodoma, kwanza kwa kutekeleza maelekezo lakini mmetekeleza kwa ubunifu,  kwa kuboresha mambo zaidi.

"Mkoa wa Dodoma tunazungumzia utalii wa zabibu na ambao wakati wote tumetamani tuwe na maeneo maalum ambayo wakija Watalii watapata mahali kwa kujifunza 'value chain' yote ya zabibu hatua kwa hatua na hapa patakuwa mahali sahihi." alielezea Senyamule

Mhe. Senyamule aliongeza kuwa mradi huo utakuwa wa mfano wa kuigwa Nchini, na utasaidia wakulima wengine kujifunza mbinu bora za kilimo na uchakataji wa bidhaa za zabibu.

"Nisisitize kuwa hiki tunachokwenda kukifanya ni lazima kifanyike kama jambo la Mfano, jambo ambalo wakulima wengine watakuja kujifunza, raia watakuja kuchukua uzoefu, kwa hiyo sisi tufanye kitu ambacho kimebobea na kina utaalamu wa kutosha. Nafurahi kuwa wataalam wenu wameshakwenda Afrika Kusini kujifunza vitu mbalimbali, kwa hiyo naamini tutapata kitu kitu kizuri.Vijana wanasema kitu  'amazing'." Alisisitiza Senyamule

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko aliweka bayana kuwa  kwasasa kiwanda hicho kipo kwenye matengenezo na kipo mbioni kuanza uzalishaji.

"Jiji la Dodoma lilikuwa limempatia mpangaji aliyekuwa anajulikana kama CETAWICO ambaye alikuwa anafanya shughuli za uchakataji na uzalishaji wa mvinyo, kwa hiyo kwa sasa kinachoendelea hapa ni ukarabati mdogo na usimikaji wa mitambo.

Hali ilivyo  sasa baada ya hicho kiwanda kufungwa, kwa ukanda huu wa Hombolo ambao ndio wazalishaji wakubwa wa zabibu, wameathirika kwa kiasi kikubwa sana kwenye upatikanaji wa masoko, kwa hiyo utekelezaji huu utaondoa hiyo changamoto na tutaharakisha msimu ujao tutakutana nao ili tuwe tayari kuanza uzalishaji wa 'wine'." alisema Dkt. Sagamiko.

Kiwanda hicho, mara kitakapoanza kazi rasmi, kinatarajiwa  kuzalisha hadi lita milioni 1.5 za mvinyo kwa mwaka, kiwango ambacho kitachochea kwa kiasi kikubwa uchumi wa ndani kupitia ajira, soko la zabibu na mapato ya Serikali.

Mradi huo unaweza kuwa kichocheo muhimu cha maendeleo Nchini, na kuifanya Dodoma kuwa kitovu cha utalii wa zabibu Afrika Mashariki na kati.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KIWANDA CHA MVINYO KUFUFUA MATUMAINI YA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA

    October 08, 2025
  • MAFUNZO YA VIKUNDI MAALUM CHACHU YA KUBORESHA SHUGHULI ZA VIWANDA

    October 08, 2025
  • BAHI WAPEWA HEKO UJENZI MIRADI YA ELIMU

    October 08, 2025
  • “TUSIMAME IMARA JUU YA KULINDA AMANI YA NCHI YETU - RC SENYAMULE

    October 07, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.