• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

JAMII YATAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA KIKATILI

Imetumwa : December 10th, 2024

Na Sizah Kangalawe 

Habari - Dodoma Rs

Wananchi wa Dodoma wametakiwa kukemea na kuondokana na tabia za ukatili wa kijinsia unaofanyika ndani ya jamii wanazoishi ili kuandaa jamii iliyobora na yenye maendeleo kwa Taifa.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alipokuwa akizungumza na hadhira katika Kongamano la kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, lililofanyika katika ukumbi mikutano wa 'Dear Mama' jijini Dodoma.

Aidha, Mhe. Senyamule alizitaja takwimu za mwenendo wa matukio ya ukatili mkoani Dodoma,ambapo alisema kuwa kwa Mwaka 2023 (Januari - Agosti) matukio yaliyoripotiwa yalikuwa 3,012 huku watoto wakiwa ni 846 na watu wazima ni 2,166. Pia alisema kwa Mwaka 2024 (Januari - Agosti) matukio yamepungua hadi kufikia 2,352 huku watoto wakiwa 529 na watu wazima wakiwa 1,723.

Sambamba na hilo, Senyamule alitoa rai kuwa jamii iendelee kuelimishwa kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na kuwataka wananchi kutosita kutoa ushirikiano endapo kuna viashiria au ufanyikaji wa vitendo vya ukatili ili hatua stahiki zichukuliwe kwa watakaobainika.

"Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akifanya jitihada kubwa katika kutokomeza  ukatili wa kijinsia, amefanya mambo mengi baadhi yake ni ujenzi wa Shule zakutosha, utoaji wa mikopo kwa wanawake, urahisishaji wa huduma kama ya upatikanaji wa maji pamoja na uwepo wa nishati safi. Hayo yote ukiyatazama kwa undani, yamechangia kwa sehemu kubwa kupunguza matatizo hayo ya ukatili wa kijinsia" alisema Senyamule.

Senyamule alisema yupo tayari kutoa msaada na ushirikiano kwa yeyote atakayetoa taarifa katika ofisi yake kuhusu utendekaji wa matukio ya ukatili wa kijinsia.

"kila mmoja akatimize wajibu wake kwa kuhakikisha hakuna tendo la kikatili linalotendeka mbele yake, kwa kufanya hivyo tutaikomboa Dodoma" alisema Senyamule.

Ikumbukwe kuwa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Desemba kila mwaka, kwa mwaka 2024 maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yameongozwa na kauli mbiu inayosema “Kuelekea Miaka 30 ya Beijing: CHAGUA Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia”

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.