• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KANISA LATOA MICHE 74,000 YA MATUNDA KWA MKOA WA DODOMA

Imetumwa : November 16th, 2022

Kanisa la Yesu Kristo la watakatifu wa siku za mwisho lenye Makao makuu yake nchini Kenya ingawa pia lina tawi nchini Tanzania, limekabidhi msaada wa miche takribani 74,000 ya miti ya matunda mbalimbali kwa Mkoa wa Dodoma,miche ambayo imepokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule katika hafla iliyofanyika katika Kata ya Miyuji eneo la Mlimwa.

Miche hiyo ambayo ni mchanganyiko wa matunda kama vile michungwa, milimao, miparachichi na miembe, imepokelewa na inatarajiwa kugawanywa kwenye Halmashauri zote Nane za Mkoa wa Dodoma ambapo Bahi itapata miche 6,410;Chamwino miche 8,100; Chemba miche 10,000; Dodoma Jiji miche 12,500; Kondoa Mji miche 8,420; Kondoa DC miche 9,800;  Kongwa miche 11,100 na Mpwapwa miche 9,700.

Akizungumza wakati wa kupokea miche hiyo, Mhe. Senyamule amelipongeza Kanisa hilo kwa kuikumbuka Dodoma kwa msaada huo kwani utasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye kampeni ya kuikijanisha Dodoma.

“Tunalishukuru Kanisa kwa utashi huu wa kuichagua Dodoma. Wanadodoma, tuifanye miche hii ikue na kuwa miti kwani hii bado haijawa miti, inataka utayari, utashi na dhamira. Natoa wito tusimamie miche hii ikue na tuache sababu ambazo zinasababisha miche huu isikue kwani hii si mapambo bali inatakiwa ikue na kuwa miti” RC Senyamule

Pia ameongeza kuwa, kila atakayechukua miche hii, ahakikishe ameitunza na asipewe mtu asiyeweza kuitunza kwani jambo hili likitekelezwa kwa dhati, ni faida kubwa kwa Mkoa wetu. Kadhalika ametoa wito kwa Wakurugenzi wote kuhakikisha wanasimamia miche hii pamoja na kumtaka Afisa Habari kufuatilia maendeleo ya miche hii kila hatua na kupeleka taarifa mezani kwake kila mwezi.

Awali, akisaini mikataba ya makabidhiano ya miche hiyo, zoezi lililofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa Dkt Fatuma Mganga, amesema;

“Tumeingia makubaliano tunakwenda kuitunza miche hii na kuwa msaada kwenye maeneo manne yakiwemo mazingira kwani tunakwenda kukijanisha Dodoma na Halmashauri zake. Pili miti hii itasaidia kwenye lishe kwani tutapata matunda ya kutosha ambayo pia yatakua msaada kwa Watoto wetu mashuleni wataweza kupata matunda. Pia itainua uchumi kwani itazaa na tutapata matunda yatakayoongeza uchumi wa shule, familia n.k Wakati tunatekeleza mradi tutakua tunaandaa taarifa kwenda kwa wenzetu juu ya maendeleo ya miti” Dkt Mganga

Akiongea kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wakati akipokea miche hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jiji Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa jambo hili linaunga mkono dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan ya watumishi kuhamia Dodoma Pamoja na kuikijanisha. Pia ameongeza kuwa watazingatia ajenda ya kuikijanisha Dodoma kwenye soko la Machinga kwa kupanda miti pale.

Naye mwakilishi wa Kanisa hilo Bw. Ronald Kivi, amesema kuwa Kanisa limefurahi kutekeleza mradi huo hapa Dodoma kwani linafanya hivyo pia kwa mikoa mingine ikiwemo Arusha na mingine.

“Kanisa tumefurahi kufanya jambo hili na Mkoa na tunaamini tutafanya mengine mengi zaidi hapo baadae. Tunaamini miche yote itakwenda sehemu husika kwani lengo kuu ni kusaidia na kuinua jamii” Bw. Kivi

MWISHO

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.