• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KITUO CHA DAMU SALAMA KANDA YA KATI CHA ZINDURIWA DODOMA

Imetumwa : June 14th, 2023


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amezindua Jengo la Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Kati Dodoma na kuzielekeza Hospitali zote za Rufaa za Mikoa zianze mpango wa utekelezaji wa mazao ya damu, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya mchangia damu duniani yaliongozwa na kauli Mbiu "Changia Damu Changia Mazao ya Damu (plasma ) mara kwa mara”

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Juni 14, 2023 katika eneo la Itega, Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, Mhe. Kim Sun Pyo, Balozi wa Korea ya Kusini hapa nchi, Dkt. Best Magoma, Mganga Mkuu Mkoa, wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na wadau wa Maendeleo.

"Takwimu za ukusanyaji damu, zimeonesha mafanikio ya ongezeko la ukusanyaji wa damu mwaka hadi mwaka. Mwaka 2022/2023, Mpango umeweza kukusanya chupa za damu 495,600 sawa na asilimia 84 ya mahitaji ya damu nchini ikilinganishwa na chupa 366,206 zilizokusanywa mwaka 2021/2022 sawa na asilimia 67 ya mahitaji". Amesema Mhe. Ummy

Aidha, Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa vituo vya afya ili kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na kuvuja damu wakati wa kujifungua.

"Takwimu zinaonesha kwamba, Tanzania ina vifo 556 vya akina mama Wajawazito (Maternal deaths) katika vizazi hai 100,000. Na kisababishi kinachoongoza katika vifo hivi ni kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua (Postpartum haemorrhage) ambayo inachangia kwa takribani asilimia 43 ya vifo vyote”

"Kwanza, Kila hospitali ya Rufaa ya Mkoa ianze utengenezaji wa mazao ya damu ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa plasma (FFP) kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama hawa. Pili, Vituo vyote vinavyotoa huduma za mama na mtoto vinunue majokofu kwa ajili ya kuhifadhia mazao damu aina ya plasma.

"Idara ya Mama na Mtoto iwezeshe Mpango wa Taifa wa Damu Salama kufanya mafunzo ya matumizi ya sahihi ya damu hasa matumizi ya plasma kwa akina mama wanaovuja damu nyingi wakati wa kujifungua kwa kuwa tafiti zinaonyesha matumizi yasiyo sahihi ya damu yanayofikia asilimia 67.2 hupelekea uhitaji wa kufanya mafunzo kwa watoa huduma za afya wanaohusika kuwaongezea damu wagonjwa."Amesisitiza Mhe.Ummy

Aidha, Wizara ya Afya imezindua kanzidata kwa ajili ya Wachangia damu wenye makundi adimu ya damu (Rh negative). Kanzidata hiyo itawasaidia Wachangia damu wenye makundi adimu kutambuana na kusaidiana pale mmoja wao anapokuwa na uhitaji wa damu ya kundi adimu. Vilevile, kanzidata hii itauwezesha Mpango kuweza kuratibu upatikanaji wa damu kunapokuwa na dharura mahali popote nchini.

Naye. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameendelea kuishukuru Serikali ya Awamu wa sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha sekta ya Afya na kwa kuchagua Mkoa wa Dodoma Kanda ya kati kuweza kujenga Jengo la Damu Salama, hii itawezesha Wananchi kuweza kupata matibabu kwa haraka na kuokoa maisha ya wengi.

Vilevile, katika Maadhimisho hayo idadi ya vyeti 17 viligawiwa kwa wachangiaji Bora wa Damu nchi nzima na tuzo. Bw. Emmanuel Lembe alipatiwa tuzo na KOICA kwa kuchangia damu zaidi ya mara nyingi 94,Timu ya Mpira wa Mguu ya The Dar es Salaam Young African wamechangia chupa 727, Shule ya Sekondari Lyamungo chupa 620, Exim Benki na Azam Media .

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.