• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAFUNZO YA VIKUNDI MAALUM CHACHU YA KUBORESHA SHUGHULI ZA VIWANDA

Imetumwa : October 8th, 2025

Na Elizabeth S. Dai – DODOMA

Mafunzo kupitia mfumo jumuishi wa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu yametajwa kuwa chachu muhimu ya kuboresha shughuli za kiuchumi kwa wanufaika wa vikundi hivyo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu, wakati akifungua mafunzo kwa vikundi vilivyokidhi vigezo vya kupata mkopo wa asilimia 10, katika ukumbi wa Nala Hotel, Jijini Dodoma, tarehe 8 Oktoba 2025.

Dkt. Kazungu amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza ujuzi na maarifa kwa wanavikundi ili waweze kuendesha miradi yao kwa tija na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku.

“Naamini mafunzo haya yatawawezesha kuboresha shughuli zenu za kiuchumi na pia kupata mbinu bora za kutatua changamoto za uendeshaji wa miradi ya vikundi,” alisema Dkt. Kazungu.

Aidha, amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwa kujitokeza kwa wingi na kuonyesha dhamira ya dhati ya kuboresha maendeleo ya vikundi vyao.

“Nawapongeza wanavikundi wote kwa kuhudhuria mafunzo haya ya awamu ya pili. Nimeelezwa kuwa jumla ya vikundi 14 vyenye wanachama 54 vimeshiriki, jambo linaloonyesha mwamko mkubwa wa kujifunza,” aliongeza Dkt. Kazungu.

Kwa upande wake, Meneja wa Tawi la LAPF, Bw. Honest Mushi, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuboresha mifumo ya utoaji wa mikopo, hatua iliyowezesha Benki ya CRDB kufikia halmashauri tano ikiwemo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mafunzo hayo yameandaliwa na CRDB Foundation kwa lengo la kuwajengea wanavikundi uwezo katika masuala ya uendeshaji na usimamizi wa miradi pamoja na namna bora ya kukopa na kurejesha mikopo.


#DodomaFahariYaWatanzania

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KIWANDA CHA MVINYO KUFUFUA MATUMAINI YA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA

    October 08, 2025
  • MAFUNZO YA VIKUNDI MAALUM CHACHU YA KUBORESHA SHUGHULI ZA VIWANDA

    October 08, 2025
  • BAHI WAPEWA HEKO UJENZI MIRADI YA ELIMU

    October 08, 2025
  • “TUSIMAME IMARA JUU YA KULINDA AMANI YA NCHI YETU - RC SENYAMULE

    October 07, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.