• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MABALOZI WASHAWISHIWA KUWEKEZA DODOMA KWANI INA VIGEZO VINAVYOJITOSHELEZA

Imetumwa : May 27th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania wamehamasishwa kuzishawishi nchi hizo kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma kutokana na Mkoa huu kuwa na vigezo vyote muhimu na vinavyojitosheleza kuvutia wageni ikiwemo ardhi ya kutosha kwa ajili ya biashara na uwekezaji inapatikana na uhitaji wake ni mkubwa.

Hayo yamebainishwa na Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Mahmoud Thabiti Kombo alipokua akizungumza na Mabalozi hao kwenye Mkutano na baadae ziara iliyopewa jina la ‘Diplomatic Capital City Tour’ leo Mei 27, 2025 katika Ukumbi wa Sephil Sepphire Jijini humu.

“Dodoma kuna fursa za biashara na uwekezaji kwa kuwa ina ardhi ya kutosha yenye maji au uwezo wa kuchimba visima, utalii, Mahoteli na uhitaji wake ni mkubwa sana. Maeneo yanayoonekana kuwa mbali na mji, muda si mrefu hayataonekana kuwa mbali kwa sababu mahitaji ya makazi na Mahoteli ni makubwa mno hivyo changamkieni fursa hii”.

Aidha, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali katika kipindi hiki cha miaka minne imewekeza zaidi ya shilingi Trilioni 5.1 kwenye uboreshaji wa elimu ambapo takribani shule za Msingi 1,399 na shule za sekondari 1,044 zimejengwa sambamba na ujenzi wa Mabweni, Maabara pamoja na nyumba za walimu.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amezungumzia miradi ya kimkakati inayotekelezwa Mkoani hapa ambayo inaufanya kuwa na hadhi ya Makao Makuu ya nchi na kuwa chachu ya kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi.

“Serikali imewekeza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba, ujenzi wa Reli ya mwendo kasi (SGR), ujenzi wa barabara ya mzunguko wan je, Kiwanja cha ndege cha Kimataifa Msalato, miundombinu ya umwagiliaji, kituo cha kupozea umeme kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere ambapo miradi yote imegharimu zaidi ya shilingi Trilioni 10”.

Akizungumza baada ya hafla hiyo, Balozi wa China nchini Mhe. Dr. Lu Youqing, amesema nchi yake inaunga mkono maendeleo ya Tanzania na ameshawishi makampuni ya nchini mwake kutembelea Dodoma na kuleta shughuli zao za kibiashara hapa ili kupata maendeleo ya kibiashara pamoja.

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko ametumia wasaa huo kuelezea juu ya mradi unaotarajiwa kutekelezwa Hombolo kwa kuufanya kuwa Mji wa Kidiplomasia kutokana na uwepo wa Ziwa Hombolo ambalo lipo umbali wa Km 70 kutoka Dodoma Mjini na eneo hilo ni la kimkakati kwani lipo karibu na Mji wa Serikali, eneo la Mabalozi pia kiwanja cha ndege cha Msalato.

Sanjari na Mkutano huo, Mabalozi hao walipata fursa ya kutembelea miradi kadhaa ya kimkakati kwa kuanzia kwenye huduma za afya ambapo walitembelea Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa na kujionea huduma za kisasa zinazotolewa, walitembelea ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba na mwisho walitembelea mradi wa Kiwanja cha Ndege Msalato.

 ‘ Capital City Diplomatic Tour’, imeandaliwa kwa kutambua mchango wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejenga mahusiano mazuri na nchi zote Duniani,hali inayowafanya wafurahie kuja Tanzania, na haya yote wamekua wakiyafanya katika nchi mbalimbali hivyo sasa ni zamu ya Dodoma.

Kaulimbiu: “Dodoma ipo Tayari kwa Ajili yenu (Dodoma Were Ready For You)”


#takedodomatotheworldandbringtheworldtododoma

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.