• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

" Machinga Complex- Dodoma, Mfano wa Kuigwa" Mhe. Seleman Jafo

Imetumwa : July 26th, 2022

Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Said Jafo (Mb) ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea  Soko la Machinga Complex lililopo jijini Dodoma. Mhe. Jafo amesema kuwa pamoja na kutembelea soko nimekuja kuona kama mambo ya mazingira yamezingatiwa katika  Ujenzi wa Soko hili la Machinga Complex.

“Hii ni pamoja na kuangalia mambo makubwa matatu, kuangalia matumizi ya nishati,maana nimesikia kutakuwa na wamachinga ambao watakuwa wanapika vyakula  hivyo nimekuja kuona kama watatumia nshati ya aina gani kama kuni au mkaa  au gesi, pia  nimekuja kuona mfumo wa maji safi na maji taka, pamoja na mfumo wa kuhifadhi maji ya mvua.  Aidha nimekuja kuona jinsi ambavyo mtahifadhi taka maana Wizara yangu inashughulika na mambo yote hayo “ Amesema Mhe. Jafo.

Akielezea hali ya ujenzi wa Soko hilo ambao umezingatia mazingira kwa kiasi kikubwa,  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw.Dickson Kimaro  amemshukuru Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira kwa kutembelea eneo hilo  na kumhakikishia kuwa ujenzi wa soko hilo umezingatia masuala yote ya kujali mazingira kwani  Wapishi hawatatumia kuni wala mkaa badala yake watatumia gesi na tayari kuna sehemu maalumu za kuhifadhia  mitungi ya gesi hizo.

Kuhusu suala la mfumo wa maji taka, bwana Kimaro amemhakikishia Mhe. Jafo kuwa  tayari kuna mfumo wa maji safi na maji taka  na  kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu sana na DUWASA. Aidha kuna maeneo matatu ya kuchomea taka, kuna  eneo la kuchomea taka ngumu,eneo la taka za chupa na eneo la  taka za karatasi na chakula. Maeneo yote haya yatatumika kuhifadhia taka kabla ya kupelekwa Dampo. Pamoja na hayo Kaimu Mkurugenzi amemhakikishia Mhe. Jafo kuwa Soko limezingatia mfumo mzuri wa kuhifadhia maji ya mvua  ambapo maji ya mvua yatakuwa yanakusanywa na kuhifadhiwa kwenye tenki  la lita 150,000.

 Nae Mkandarasi Bw. Taher Mustafa, ameonyesha kufurahishwa na ziara ya Mhe. Jafo kwani ziara za viongozi zimekuwa kichocheo kwao kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Bw.Mustafa ameeleza kuwa mafaniko makubwa katika kazi yao yamesabishwa na usimamizi madhubuti wa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma pamoja na Timu yake.

Aidha mara baada ya kupokea maelezo ya Kaimu Mkurugenzi na Mkandarasi Mhe. Jafo alitoa maelekezo kwa  Mkurugenzi wa Jiji la  Dodoma Kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,ili  asaidie upatikanaji wa natural gesi moja kwa moja.  “Wasiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC ili waje kuweka mtungi mmoja ambao watu watakuwa wanalipia. Soko hili ni  la kisasa na la mfano Tanzania, hivyo watu watafungiwa meter na kuanza kulipia  gesi kulingana na  matumizi”.Amesisitiza Mhe. Jafo.

Mhe Jafo amepongeza uwepo wa udhibiti madhubuti wa maji," Cha muhumi haya maji ya mvua yakijaa kwenye tank badala ya kuanza kufurika humu ndani  basi kuwe na njia ya kuyatoa nje.  Pia ni vyema mkapanda maua mazuri na miti na ni lazima watu wa Mazingira wahakikishe kuwa wakati wote kuna mtu muhimu wa kusimamia mazingira. Pongezi kubwa kwa mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi na mkandarasi ni vyema kuwatumia makandarasi wazawa kama hawa. Nimefarijika sana, Soko hili ni la Mfano  wengine waje kujifunza  katika kulinda mazingira".amesema Mhe Jafo

Akitoa shukrani Mkuu wa MKoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka  amemshukuru  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Said Jafo (Mb kwa kutembelea na kujionea jinsi ujenzi wa Machinga Complex unavyoendelea.Aidha Mhe. Mtaka amemwahidi Mhe.Waziri kuzingatia na kufanyia kazi maelekezo yake yote.

Mhe. Mtaka amemfahamisha Mhe. Waziri kuwa yeye na viongozi wengine wamejitahidi kuhakikisha kuwa wafanya biashara katika Soko hilo ni machinga kwani  Watu watakaokuwa hapa ni watu wa kawaida kabisaaa. “Tunataka machinga ambaye mvua jua na mvua   vyote vya kwake. Benki ya NMB imeahidi kutoa Tsh. 500,000/- kwa kila mfanya mmachinga atakayekuja hapa. Hivyo nitoe Wito kwa  Vijana wote wa machinga  ambao ni zaidi ya machinga 6000 wote waje kufanya biashara zao humu.Sitaki mtu abaki huko mtaani ” Amesisitiza  Mhe. Mtaka.

Mwisho.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.