• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

Imetumwa : May 17th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Madereva wa magari ya Serikali wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya usalama barabarani pindi wanapokuwa wakiendesha magari hayo.

 Hayo yamebainishwa Mei 17, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP George Katabazi wakati akizungumza na madereva hao kwenye kikao maalumu alichokiitisha katika ukumbi wa PGA Jijini Dodoma kilicholenga  kuzungumza nao juu ya utii wa sheria za usalama barabarani kwani baadhi yao wamekuwa wakilalamikiwa kukiuka sheria hizo.

“Kikubwa ni kuwataka Madereva wa Serikali kuzingatia sheria na taratibu zinazohusiana na usalama barabarani. Tunawakaumbusha, tunawaelimisha kuhusiana na sheria hizo, taratibu na kanuni lakini pia kuwaonya baadhi yenu ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani. Tunawakemea wale ambao kwa makusudi wanavunja sheria hizo”.

Aidha, Kamanda Katabazi ameongeza kuwa wana andaa utaratibu ambao utahusisha kuundwa makundi sogozi yatakayohusisha Viongozi wa Madereva wa Serikali katika kila Mkoa pamoja wasimamizi ambao ni Maafisa usalama barabarani  wa Mikoa husika.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa chama cha Madereva wa Serikali Bw. Issa Kisebengo amesema kuwa elimu waliyoipata kwenye kikao hicho imewasaidia kutambua majukumu na wajibu wao kwenye Utumishi wa Umma na kutoa wito kwa madereva wenzake.

“Sisi ni vioo kwa madereva wengine lakini pia tunabeba Watumishi wa Serikali, na kuna watumiaji wengine wa barabara,wote hao wanatutegemea sisi kwa usalama wao hivyo, mafunzo tuliyoyapata hapa, tusiyaache hapa hapa, tuyabebe, tuyatunze na twende tukayafanyie kazi”.

Licha ya kukumbushwa sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani, kikao hicho pia kiliambatana na mafunzo mbalimbali yaliyotolewa kwa madereva hao ili kuendelea kuwakumbusha kuhusu kuzingatia sheria hizo kwani kuwa madereva wa magari ya Serikali si kigezo cha kuvunja sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.