• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

“MFUMO WA NEST UMEKUJA KUWALINDA WAFANYABIASHARA NA FEDHA ZA SERIKALI “- RC SE

Imetumwa : October 21st, 2024

 Na. Hellen M. Minja,    

       Habari – DODOMA RS


Wasimamizi wa miradi ya maendeleo hususan Shule, wametakiwa kusimamia na kukamilisha miradi kwa wakati kwa kutumia mfumo wa manunuzi Serikalini (NeST) kwani mfumo huo unawalinda wafanyabiashara kama unavyolinda fedha za Serikali.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, Oktoba 21, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua miradi ya madarasa, shule mpya na nyumba za walimu katika shule za Sekondari Mpunguzi, Matumbulu na Miyuji ‘B’.

Miradi ya shule hizo imeonekana kuwa nyuma ya wakati huku sababu zikitolewa kuwa ni changamoto zilizojitokeza kwenye matumizi ya mfumo wa NeST hivyo, Mhe. Senyamule alitoa ufafanuzi;

“Serikali imebadili mfumo, haijaongeza wala kubadili muda wa kutoa malipo. Mfumo huu ni mzuri huenda ni zaidi ya ule  mliokuwa mkikutana ana kwa ana na kukubaliana. Huu hauna kupunguziana gharama, mkishakua tayari kutumia mfumo vizuri, vitu vinakwenda haraka kuliko bila mfumo. Serikali imeingia kwenye mfumo huu ili kuwalinda kama inavyolinda fedha za Serikali” Mhe. Senyamule

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri amewataka watendaji wa Kata kujikita kwenye usimamizi wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora, kwa kuhakikisha vifaa vinanunuliwa mapema na kuepuka visingizio vya kuelekeza nguvu kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Ziara hiyo ilianzia kwenye shule ya Sekondari ya Mpunguzi ambayo imetekeleza mradi wa ujenzi wa madarasa matatu na matundu nane (08) ya vyoo kwa kiasi cha shilingi 83,400,000/= fedha kutoka Serikali kuu na mradi huo umekamilika kwa asilimia 95.

Katika Mradi wa shule mpya ya Sekondari Kata ya Matumbulu iliyoanza kutokana na jitihada za wananchi na mapato ya ndani kiasi cha shilingi 28,000,000 na baadae kupitia mradi wa SEQUIP, Juni 23, 2024, shule ya Sekondari Mpunguzi ilipokea shilingi 544,225, 626.00 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo

Mkuu wa Mkoa alihitimisha ziara yake kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa Nyumba mbili za walimu, mabweni 2, matundu 10 ya vyoo na madarasa 4 katika shule ya Sekondari Miyuji B unaogharimu kiasi cha shilingi 454,000,000.00/= ambapo bado haujakamilika.


#kurayakosautiyako

#ujanjanikupigakura                

#dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.