• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mhe. Rosemary Senyamule, Akutana , Aongea na Wazee wa Mkoa wa Dodoma

Imetumwa : September 8th, 2022

Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amekutana na kufanya mkutano na wazee wa Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mipango ikiwa ni katika kufanya utambulisho kwao na kuwatambua wazee hao, ambao walikusanyika kutoka Wilaya zote Saba za Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza na wazee hao, Mhe. Senyamule amesema,wazee wanajua historia nzuri ya Dodoma na pia wanaweza wakabariki au kulaani hivyo amewaomba wambariki na kumpa njia ya kupita kwani yeye ni mtoto kwao na yupo tayari kusikiliza ushauri wao.

Vilevile, amesema kuwa Mkoa wa |Dodoma unaendelea kufanya maboresho mbali mbali ambapo majengo mengi yanajengwa hivi Sasa ili watanzania wakienda nchi za jirani na kujitambulisha kama anatokea Dodoma basi iwe na hadhi ya Makao makuu ya nchi.

"Tunatamani mwana Dodoma ajivunie Mkoa wake popote atakapokwenda na ndio maana tunasema Dodoma ni fahari ya wananchi kwani wageni wakija kuitembelea Tanzania tunataka wajifunze kwa vivutio wanavyo viona na kukubali kwamba kweli hapa ni makao mkuu ya nchi" Mhe. Senyamule.

Aidha,  Mkuu wa Mkoa ameelezea kuhusu fedha za mradi inayoendelea kufanyika ndani ya Mkoa wa Dodomana kutaja kiasi hicho cha fedha kama ifuatavyo Tsh. 675.0 bln zinatumika kujenga barabara ya mzunguko yaani Ring road pamoja, Tsh.221.0 bln, zinazotumika katika ujenzi  wa uwanja wa ndege wa Kimataifa eneo la Msalato.

"Kuna msongamano  kwenye Barabara zote zinazotoka Dodoma kwenda Mikoa ya Iringa, Singida, Arusha na Morogoro na Serikali imeona changamoto hiyo na kuongeza Kilometa 50 kwenda kila upande wa Barabara inayotoka nje ya Dodoma kuweka ziwe Barabara mbili mbili kila upande na fedha zimeshatolewa na mchakatao wa ujenzi wa barabara hizo umeanza na tunatarajia kuanza na barabara ya kwenda Chamwino na baadae itafuata ya kwenda Singida na nyingine zitaendela ili kuifanya Dodoma iwe ya kisasa na inayopitika kwa urahisi."

 "Kwa Mkoa wa Dodoma pekee, Serikali imetoka Shillingi Bilioni Mia mbili kumi na sita kuhakikisha Mkoa unakua na umeme wa kutosha kwasababu tunaposema makao makuu kila sehemu inatakiwa iwe imefikiwa na huduma ya Umeme ili kuwezesha kuwa na muingiliano mkubwa, hatujawahi kuwa na makao makuu ya muhimili wa Mahakama katika nchi yetu lakini kwa mara ya kwanza Makao makuu hayo yanajengwa Mkoani hapa na jengo Hilo litagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni Mia moja na ishirini na sita na ni jengo la kisasa hasa" ameongeza Mhe. Senyamule.

Kabla ya kufunga kikao hicho, Mhe. Senyamule hakusita kutoa shukrani zake za dhati pamoja na pongezi  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa ni Rais wa tofauti,nchi nyingi zilipata fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Uviko-19 lakini kwa nchi yetu, Mhe. Rais aliona ni vyema kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo hasa kwenye sekta za Elimu na Afya.

Mkoa wa Dodoma una changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji ambapo bila kimiminika hicho, mambo mengi hayataweza kufanyika,kw kutambua hilo, Serikali imeanza mchakato wa kuhakikisha Dodoma inapata maji ya uhakika ikiwa ni mipango ya mda mfupi, mipango ya muda wa kati na mipango ya endelevu.

Wakizungumza Wazee wa Dodoma ambao walieleza kuwa mtu yeyote mwenye umri wa 60 na kendendelea anaweza kujiunga na baraza la wazee,wazee hao wamshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwani wamepata Vitambulisho ambavyo vinawasaidia na kuwapatia wepesi katika upatikanaji wa huduma mbalimbali muhimu.

Wakielezea changamoto wanazokalibiana nazo Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa wa Dodoma Bw.Petro Mpolo amesema kuwa bado wazee wanatozwa kodi za ardhi na kodi za majengo.Wengine bado wanalipia matibabu na kama nyumba ina umeme wanakatwa  kodi ya majengo katika malipo ya umeme na baadi ya wazee nyumba zao bado hazina  umeme.Kupiti mwenyekiti wao Wazee wa Dodoma wameomba kupatiwa Ofisi, kupatiwa Semina elekezina kuomba kushirikishwa kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa hasa kutoka kwenye Halmashauri.

Akizungumza Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Dodoma, Mzee. Peter Mavunde , amemshukuru Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule kwa kuwapa heshima kubwa Wazee wa Dodoma nao wanamkaribisha kwa mikono miwili, karibu Dodoma. Mzee Mavunde ametaja mambo matano am bayo amemtaua Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuzingatia ambayo ni Ujenzi wa Uwanja wa ndege  wa Kimataifa wa Msalato na Kumtaka atoe maelekezo kwa wahusika ili elimu itolewe kwa wananchi juu ya mradi huo,Ujenzi wa uwanja wa mpira, Kuboresha jiji la Dodoma na liwe safi mazingira  yawe safi, Ujenzi wa Makumbusho ya Mwl. Nyerere yajengwe pamoja na Uboreshaji wa huduma za jamii kazi ni njema na kazi hiyo itunzwe na iwafaidishe watanzania.

Aidha Mzee Mavunde ametaja Changamoto zinazowakabili wazee kwa kusema “tunaambiwa kuwa Uzee ni dawa lakini hatuna sera ya wazee, sera iwepo na itambulike, changamoto katika suala la dawa pia hakuna mwongozo maalum wa majukumu ya wazee katika jamii.Kwa niaba ya wazee wa Dodoma Mzee Mavunde ametoa ombi maalum kuwa maeneo ya kale katika mji wa Dodoma yahifadhiwe kama historia kwa Mfano eneo la Kikuyu ambapo Tembo alididimia Idodomya hilo eneo litunzwe na lipewe hati, eneo la mti mkubwa wa kunyongea,Ofisi ya Waziri mkuu, St. Johns, Nyerere Square itunzwe na paonyeshe historia ya Mwl. Nyerere. Miziki inapingwa mpaka usiku wa manane na kupelekea wazee kukosa usingizi tunaomba mambo haya yadhibitiwe.Uwanja wa barafu upewe heshima kwa kujengwa upya na kukarabatiwa upya.Matukio ya mauJi ni mengi tunaomba leo utupe maelekezo tudumishe amani na usalama. Zao la Zabibu kutafutwe maeneo yenye rutuba, maoneo  ambayo zabibu inaweza kupandwa. Suala la viwanda lipewe kipaumbele .Kama Baraza la wazee tutaendele kuisaidia ilani yetu ya CCM”.

Mwenyekiti wa Machief Mkoa wa Dodoma Chief Bilinji amemweleza Mhe. Rosemary Senyamule kuwa wanaimani Na Mkuu wa Mkoa na kuahidi ushirikiano wa hali na mali.

Nae Mzee Philip Mangula (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi) ambaye alikuwa mshiriki wa kikao hicho ameeleza kuwa anauzee wa miaka 21 kwa ni uzee unaanza mtu akiwa na miaka 60 ikimaanisha ana miaka 81.Mzee Mang’ula amewakumbusha wazee wenzake kuwa Usemi wa ‘Kazi Iendelee’ unamaanisha kwamba tunapashwa kuienzi Kazi iliyoanzishwa na Rais wa awamu ya Tano ambayo inaendelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeorodhesha  yatakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano. Mkuu wa Mkoa umefanya vizuri sana kujua wazee wa Dodoma wanataka nini”.Amesema Mzee Mangula.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.