• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MHE. SENYAMULE AKABIDHI ZAWADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Imetumwa : December 24th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo tarehe 24 Desemba 2022 amekabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya  katika  kituo cha Safina  kilichopo Ntyuka Jijini Dodoma kwa niaba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Mchele, Unga wa Ngano, Sabuni, Sukari, Mafuta, vinywaji pamoja na mbuzi wawili. Amesema zawadi hizo ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watoto katika kipindi hiki cha sikukuu.

Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuma salamu za Upendo na kuwaomba watoto hao kukua katika maadili  ya kumpendeza Mungu na wanadamu.

“Lengo na dhumuni la Mhe. Rais ni kuona watoto wanasheherekea sikukuu kwa furaha na amani, kumbukeni kuwa chochote anachokifanya ni kwaajili ya watanzania wote ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa ili watoto mpate elimu bora na kuongeza kiwango cha utafulu, hivyo mkiwa  darasani msikilize mwalimu na mkirudi kituoni muda wa jioni jisomeeni” Alisisitiza Mhe. Senyamule.

“Chochote unachokifanya fanya kwa bidii kila mtoto ana ndoto na malengo yake ya baadae, Serikali inatambua mchango wenu ndio maana Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kutoa zawadi hizi za vyakula  na kiasi cha fedha ili wote mfurahie sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya. Mhe. Senyamule aliongezea.

Mhe. Senyamule amewashukuru waangalizi wa watoto hao kwa kujitoa kwao kuwalea katika maadili mema na kumuomba Mungu kuendelea kuwabariki Walezi na wahudumu wengine katika malezi ya watoto hao.

“Jukumu lenu ni pamoja na kuhakikisha watoto hawa wasoma ili kuyatumia madarasa yanayojengwa na Serikali  chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili tuwe na kizazi chenye maadili mema ya kitanzania na ndoto za kutimiza malengo ya watoto wetu” Alifafanua Mhe. Senyamule.

Aidha mlezi wa kituo cha Safina Bi. Neckson William ameishukuru Serikali kwa kutoa zawadi za sikukuu kwa watoto.

“Tunaishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutusaidia kituo cha Safina tumefurahi sana kwakuwa tuna watoto ambao pia wapo nje ya Safina. Kituo kinawatoto kuanzia miaka miwili na mwaka huu tumefanikwa kupeleka Chuo Kikuu watoto wawili” Alisisitiza Bi. William

Kituo cha Safina kilianzishwa mwaka 2004 na kina jumla ya watoto 40, wavulana 35 na wasichana 5 pia kitua hicho kinawasaidia watoto ambao wanatoka katika mazingira magumu.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.