• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MIAKA 63 YA UHURU WA TANZANIA BARA;RC SENYAMULE ASISITIZA AMANI NA USALAMA

Imetumwa : December 9th, 2024

 Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Amani na usalama vimetajwa kuwa msingi wa mafanikio ya Mwananchi mmoja mmoja na Nchi nzima kwa ujumla. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika Kimkoa katika Kata ya Makutupora, Jijini Dodoma.

Mhe. Senyamule aliyekua Mgeni rasmi katika hafla hiyo, amesema Tanzania inajivunia amani na usalama kutoka kwa Waasisi wa Uhuru, na ndio sababu ya maendeleo makubwa tunayoyaona leo hii hasa kwa Mkoa wa Dodoma.

“Tumeshuhudia muundo wa Nchi yetu ulivyo na ushirikishwaji mkubwa wa Wananchi. Mkoa wa Dodoma tunatekeleza kwa vitendo na ndio sababu ya kupata maendeleo haya makubwa. Amani na usalama wa Nchi, ni msingi wa mafanikio, tuvitunze kwa kufanya mambo kwa utaratibu” Mhe. Senyamule

Kadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri, amesema "Uhuru wa Nchi yetu unaendelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia vizuri vyombo vya Ulinzi na Usalama, hivyo tunajivunia kuwa na Viongozi madhubuti kwenye awamu zote sita za Uongozi wa Serikali Kuu".

Sherehe hizo zilitanguliwa na zoezi la upandaji miti katika eneo la Jeshi la JKT Makutupora Kikosi 834, ambapo Mkuu wa Mkoa wa  Dodoma aliongoza zoezi hilo kwa kufanikisha kupandwa kwa miti 800 katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, amesema;

“Tumeshiriki kupanda miti tangu 2017 tulipozindua kampeni ya ‘Dodoma ya Kijani’ katika eneo la Mzakwe ambapo TFS na Jiji la Dodoma tuliingia mkataba wa kuifanya Dodoma ya Kijani, na kuanzia hapo huwa tunatoa miche bure kwa ajili ya kupanda kwenye maeneo yaliyochaguliwa” Prof. Silayo

Hata hivyo, miongoni mwa wadau walioshiriki katika Maadhimisho hayo ndani ya Mkoa wa Dodoma ni mwendesha baiskeli anayejulikana kwa jina la Mwl. Wenseslaus

Justine Lugaya ambaye alianzia safari yake  Mkoani Kigoma kwa lengo la kuenzi maadhimisho hayo ambapo alifanikiwa kufika Jijini Dodoma usiku wa kuamkia Desemba 09, 2024.

Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yaliasisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere mwaka 1961 wakati Tanzania ilipopata Uhuru wake wa Kikatiba kutoka kwa Waingereza. Kuanzia hapo iliweza kujitawala yenyewe na kudumisha amani na utulivu hadi sasa.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu”


#miaka63yauhuruwatanzaniabara

#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu                              

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.