• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MIRADI YA BARABARA IKIDHI VIPAUMBELE VYA MKOA-RC SENYAMULE

Imetumwa : March 7th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka Wataalam wanaoshughulika na usimamizi wa miradi ya maendeleo hususan miundombinu ya barabara, kuhakikisha inakidhi vipaumbele vya Mkoa wa Dodoma hasa katika kuinua uchumi wa wananchi wa Mkoa huu.


Hayo yamebainishwa wakati wa kikao cha pili cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dodoma 2024/2025, kilichofanyika Machi 06, 2025 katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Jengo la Mkapa Jijini humu ambacho kimelenga zaidi kujadili mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka mpya wa fedha 2025/2026.


“Sisi kama Mkoa, tunavyo vipaumbele ambavyo tunatamani miradi hii ivipe uzito stahiki, Wataalam tunaendelea na mchakato wa bajeti kwa sasa. Tunategemea kuona mabadiliko ya miundombinu hii kuimarika kwenye Mkoa wetu lakini mwisho wa siku miundombinu ni uchumi, huduma za wananchi zitaimarika, na baadae uchumi wa wananchi utaimarika pia”. RC Senyamule.


Kadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, ameshauri kutumika Sheria ya kutoa kwa jamii kwa kampuni zinazopata Zabuni za ujenzi wa barabara kwa dhana ya kuondoa changamoto za kiusalama barabarani kwa kuwezesha uwekaji taa za barabarani pamoja na kamera, hatua ambayo itaufanya Mkoa kuwa nadhifu na kudhibiti matukio ya kihalifu.


Akiwasilisha mapendekezo ya bajeti mpya 2025/2026 kutoka kwa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Meneja Mkoa wa Dodoma,Mhandisi Zuhura H. Amani, amesema upande wa matengenezo ya barabara kuu na zile za Mkoa, wamependekeza jumla ya shilingi Bilioni 16.662 ambayo ni sawa na bajeti ya mwaka huu na kwa upande wa miradi ya maendeleo, wamependekeza jumla ya shilingi Bilioni 1.128.


Kwa upande wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA Mkoa wa Dodoma, wamewasilisha mapendekezo ya Bajeti shilingi 33,465,594,956.64 inayolenga baadhi ya vipaumbele kama kuboresha barabara zilizopo, zinazolenga mzunguko wa magari katika mtandao wa barabara, kuboresha mitaa mikuu, kusaidia maeneo kufikika wakati wote na kufanikisha kiwango sahihi cha huduma ya usafiri kwa barabara za vijijini.


Kikao hicho pia huambatana na taarifa za utekelezaji wa miradi ya maji Mijini (DUWASA) na ile ya Vijijini (RUWASA), taarifa za miradi na upatikanaji wa umeme katika Mkoa kutoka TANESCO ambapo taasisi hizo zote zimekuja na mapendekezo ya bajeti kwa mwaka mpya wa fedha 2025/2026.


Hata hivyo, baadhi ya maazimio yaliyofikiwa na kikao hicho ni pamoja na Mkoa kuunda Tume itakayofanya ufuatiliaji wa fedha za miradi ya Barabara za kimkakati, vipaumbele vya barabara vijumuishe zile zinazoingia katika maungio ya SGR, Kiwanja cha ndege cha Kimataifa Msalato na maeneo ambayo miundombinu ya kutoa huduma za jamii inatekelezwa.




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.