• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA DODOMA WABAINISHA VIPAOMBELEE VYAKE 2024

Imetumwa : January 18th, 2024

Mkoa wa Dodoma umeweka wazi vipaombele vyake kwa mwaka 2024 ikiwa ni pamoja kuimarisha sekta ya kilimo inayochangia asilimia 40 ya pato la Mkoa huku sekta nyingine zikiwa Utalii, madini, Elimu, viwanda, usafirishaji pamoja na kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa leo Januari 18, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akifungua kikao na viongozi wa dini wa Mkoa wa Dodoma wenye lengo la kushirikiana katika kufikia vipaombele hivyo.

"Rais wetu amefanya kazi kubwa na ya kipekee kwa kuwa anajali watu wa chini. Serikali imetoa kiasi cha jumla ya Shilingi Bilioni 95 kwa ajili ya kutekelezwa miradi mbalimbali ya Kilimo kwenye Halmashauri za Chamwino ambapo kuna miradi mitatu, Mpwapwa mradi 1 na Bahi mradi 1. Miradi hii Ina lengo la kuimarisha kilimo kiwe cha kisasa zaidi kwa kuwa cha umwagiliaji kwa mwaka mzima.

"Tunahitaji Dodoma iwe kitovu cha usafirishaji ili kuinua Uchumi kwa haraka na kuwa Mji wa kimkakati kwani hali ya Uchumi bado si ya kuridhisha. Kwenye Utalii, tuna vivutio vingi sana na tunahitaji Sasa wawekezaji wakubwa kwa ajili ya kujenga Hoteli zenye hadhi ya nyota 5 ambazo zitawezesha kupokea wageni wenye hadhi kubwa kutoka mataifa tofauti tofauti." Ameeleza Mhe. Senyamule

Akiwasilisha taarifa ya Elimu kwa Mkoa wa Dodoma, Afisa Taaluma Mkoa Mwl. Justin Machela amesema Mkoa wa Dodoma umejiwekea Mkakati wa Elimu 2024 wenye lengo la kuinua ufaulu wa Mkoa.

"Mkakati wa Elimu Mkoa umejikita katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni kwani hii itasaidia kutokomeza utoro na kuimarisha mahudhurio kwa wanafunzi. Kwenye matokeo ya mitihani ya Taifa tumedhamiria yafanane na hadhi ya makao makuu ya nchi. Elimu ya msingi ufaulu ufikie asilimia 95, kidato cha 4 ufikie asilimia 65 kwa kupata madaraja ya I -111 huku kidato cha 6 yafikie asilimia 100 kwa ufaulu wa madaraja 1-11 tu.

"Aidha, mahudhurio ya wanafunzi wapya kwa muhula wa 2024 ambapo kwa madarasa ya awali waliandikishwa wanafunzi 64,707 walioripoti ni 54,060 sawa na asilimia 63.5, darasa la kwanza waliandikishwa ni 79,099 walioripoti ni 65,765 sawa na asilimia 56.92 hivyo mahudhurio yanaridhisha " Amesema Mwl. Machela.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AFUNGUA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

    May 18, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.