• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA DODOMA WAJINOA KUIBUA WAGONJWA 1,930 WA KIFUA KIKUU

Imetumwa : January 16th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Kufuatia uzinduzi wa Mpango harakishi wa  kuibua wagonjwa wa Kifua kikuu katika Halmashauri 76 za Mikoa 9 nchini uliozinduliwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama Januari 06, Mkoa wa Dodoma umeanza maandalizi ya zoezi la kuibua wagonjwa 1,930 waliokosekana mwaka 2024 kwa kufanya mafunzo ya siku tatu kwa wataalamu wanaoshughulika na huduma za ugonjwa huo kwa ngazi zote.

Mafunzo hayo ya siku tatu ambayo leo Januari 16, 2025 yamefanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Golden Crown Jijini Dodoma, yameongozwa na Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Peres Lukango.

“Lengo ni kutafuta wagonjwa 1,930 waliokosekana mwaka 2024, Mkoa unafanya maandalizi ya zoezi hilo litakaloanza tarehe 20, mafunzo tunayoyafanya leo ni sehemu ya kuandaa wataalam watakaohusika na zoezi hilo. Baada ya mafunzo haya tutakua na zoezi la kukamilisha vitendea kazi kwa kila Halmashauri zitakazohusika na zoezi” Dr. Lukango.

Miongoni mwa wadau wanaosimamia mafunzo na zoezi zima ni Naibu Meneja Mpango wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Wizara ya Afya Dr. Liberate Mlech ambaye amewaambia washiriki kuwa mafunzo na nyenzo watakazozipata hapo zitafanikisha lengo la kuwapata wagonjwa hao kama ilivyokusudiwa kwani hii ni vita na nyezo hizo ndio silaha.

Kwa upande mwingine, Mshauri wa zoezi la kuibua wagonjwa wa Kifua Kikuu Dr. Deus Kamara, amesema hii ni kampeni ya tofauti kwani inahusisha kutafuta wagonjwa ambao hawaonekani. Inahitajika mikakati ya kikamilifu ili kutafuta mtu ambaye haonekani hivyo, Serikali ina dhamira kubwa ya kuhakikisha kwamba hili linatendeka.

Wataalamu wanaopatiwa mafunzo ni wale wa kutoa dawa za wagonjwa wa Kifua Kikuu, wahudumu ngazi ya jamii na wataalamu wa takwimu. Zoezi hilo litafanyika kwenye Halmashauri 7 kati ya 8 za Mkoa wa Dodoma ambazo ni Dodoma Jiji, Chamwino, Bahi, Kondoa Mji, Kondoa DC, Mpwapwa na Kongwa. Chemba haitahusika na zoezi hilo kutokana na takwimu kuonesha kuwa inafanya vizuri katika uibuaji wa wagonjwa.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu                               #mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.