• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA DODOMA WAZINDUA SOKO KUU LA MADINI YA DHAHABU NA VITO VYA THAMANI MEI 19, 2019

Imetumwa : May 19th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge Mei 19, 2019 amezindua Soko la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani humo na kutoa Rai kwa wachimbaji wadogo kuhakikisha wanatumia soko hilo kufanya biashara ya madini na kunufaika nalo na kuachana mara moja na kufanya biashara haramu ya madini na kutorosha madini hayo au kukwepa kodi na kuwa wakifanya hivyo watakumbana na hatua kali za kisheria 

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na viongozi wengine wa Mkoa na Tume ya Madini, wakikata utepe kuzindua Soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani Dodoma Mei 19, 2019

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na viongozi wengine wa Mkoa na Tume ya Madini, wakikata utepe kuzindua Soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani Dodoma Mei 19, 2019

Afisa Madini Mkazi Dodoma Ndg. Jonas Mwano (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya masuala ya miamba ya madini kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na viongozi wengine wa Mkoa na Tume ya Madini, wakati wa uzinduzi wa Soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani Dodoma Mei 19, 2019

Afisa Madini Mkazi Dodoma Ndg. Jonas Mwano (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya masuala ya miamba ya madini kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na viongozi wengine wa Mkoa na Tume ya Madini, wakati wa uzinduzi wa Soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani Dodoma Mei 19, 2019

Shughuli za usafishaji wa madini na uchakataji wake zikiendelea kwenye Soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani la Mkoa wa Dodoma, Mei 19, 2019

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akioneshwa madini ya dhahabu ambayo yanauzwa kwenye Soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito Mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa soko hilo Mei 19, 2019, wengine ni viongozi wa Mkoa na Tume ya Madini. 

Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Tume ya Madini wakikagua Soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa soko hilo Mei 19, 2019

Picha ya pamoja baina ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na viongozi wengine wa Mkoa na Tume ya Madini wakati wa uzinduzi wa soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani Dodoma Mei 19, 2019

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akiagana na viongozi na wadau wa madini Mkoani Dodoma mara baada ya  kukamilika kwa uzinduzi wa soko Kuu la Madini ya Dhahabu na Vito vya thamani Mkoani Dodoma Mei 19, 2019


HOTUBAYA MGENI RASMI DKT. BINILITH S. MAHENGE MKUU WA MKOA WA DODOMA KWENYEHALFA YA UZINDUZI WA SOKO LA 

MADINIMKOA WA DODOMA TAREHE 19 MEI, 2019 


Prof.Idris Kikula, Mwenyekiti wa Tume ya Madini; 

KatibuTawala wa Mkoa;

Wajumbewa Bodi ya Tume ya Madini;

Viongoziwa CCM Mkoa na Wilaya,

Wajumbewa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma,

Wakuuwa Wilaya; 

MakatibuTawala Wasaidizi Sekretarieti ya Mkoa;

MakatibuTawala wa Wilaya;

Wajumbewa Kamati za Ulinzi na Usalama wa Wilaya;

Wenyevitiwa Halmashauri za Wilaya;

Wakurugenziwa Halmashauri; 

Watendajiwa Wizara ya Madini na Tume ya Madini;

Viongoziwa Dini; 

Wawakilishiwa wachimbaji Madini; 

Wanahabari;

WageniWaalikwa; 

Mabibina Mabwana;

Salaam.

NduguWananchi,

Kwanzakabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwakutuwezesha sisi sote kuwa na afya njema na kutuwezesha kusafirisalama hadi mahali hapa na kuwa sehemu ya tukio hili muhimu na lakihistoria la kuzindua Soko la Madini Mkoa wa Dodoma.

Natoashukurani zangu kwa Washiriki wote mlioitikia kuhudhuria tukio hilimuhimu. Uwepo wenu hapa unaonesha utayari wenu wa kuunga Mkono azmaya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli zakuendeleza Sekta ya Madini Nchini. Aidha, shukrani za kipekeeziwaendee waandaaji wa hafla hii kwa kunialika kuwa mgeni rasmi.Nichukue fursa hii kutoa pongezi kwa uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwakazi nzuri mnayoifanya katika kutekeleza maelekezo yaliyotolewa naMhe. Rais ya kuanzisha masoko ya madini hususan katika maeneo yoteyanayochimba madini nchini.

NduguWananchi,

Tanguiingie madarakani, Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikisisitizadhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaishaWatanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa. Aidha,Serikali imeendelea kutekeleza maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi yaChama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020 ambayo inaitakaSerikali kubuni na kutekeleza mikakati mahsusi itakayowezeshakupunguza au kukomesha kabisa vitendo vya utoroshaji madini nabiashara haramu ya madini nchini.

NduguWananchi,

Kwakuzingatia hilo, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutoakipaumbele katika kulinda rasilimali za madini na kuhakikishazinawanufaisha Watanzania. Juhudi zilizofanyika ni pamoja na kutungwakwa Sheria Namba 5 ya Mwaka 2017 iliyohusu umiliki wa Maliasili;Mapitio ya Sheria Namba 6 ya Mwaka 2017 yaliyohusu majadiliano kuhusuMasharti hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi na marekebisho yaSheria ya Madini Sura 123. Aidha, Serikali imefuta baadhi ya tozoambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara ya madini hususaniwachimbaji wadogo. Miongoni mwa tozo ambazo tayari zimefutwa ni Kodiya Ongezeko la Thamani (VAT) asilimia 18 na Kodi ya Zuio (withholdingtax)ya asilimia 5 kwa Wachimbaji Wadogo. 

NduguWananchi,

Serikaliinatarajia kuwa kufutwa kwa kodi na tozo hizo kutapunguza utoroshwajiwa madini; kutasaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitiauanzishwaji wa masoko ya madini; kupunguza gharama za uendeshaji washughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato kwa nchi.Nitoe wito kwa wachimbaji wote wadogo kwamba endeleeni kushirikianana Mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yenu kwakufuata Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewana Serikali. 

NduguWananchi,

Serikaliinachukua hatua zote hizo si kwa lengo jingine bali kuziba mianyaambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi, nahivyo, kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katikamaeneo mengi ya nchi yetu. Napenda kuwahakikishia kwamba Serikaliimejipanga vema katika kuhakikisha vikwazo vyote vilivyomo katikamnyororo wa biashara ya madini vinaondolewa kwa lengo la kukuza sektahii na kuwanufaisha Watanzania mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. 

NduguWananchi,

Mkoawa Dodoma umebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali ambayo niDhahabu, Shaba, Nickel, Vito (Chrysoprase, Moonstone, Sunstone,Quartz/Quartzite na Ruby), madini ujenzi (Mchanga, Mawe, Vifusi naKokoto) na madini yanayotumika viwandani (Jasi, Chuma, Soapstone,Feldspar na Calcite). Shughuli za uchimbaji madini ziliongezekakatika miaka ya 2003 kutokana na ongezeko la waombaji wengi wa leseniza uchimbaji wa dhahabu kwa Halmashauri za Kondoa, Chemba, Chamwinona Bahi na Vito kwa Halmashauri za Mpwapwa, Kongwa na Chamwino.Wastani wa uzalishaji wa dhahabu kwa mwezi ni zaidi ya kilo tatu (3)kwa Wachimbaji Wadogo. Kutokana na wingi wa shughuli za madini katikaMkoa wa Dodoma na mchango wake kwenye Pato la Taifa, Serikali imeamuakuanzisha Soko hili tunalolizindua hii leo. 

NduguWananchi, 

Uanzishwajiwa Soko la madini unatarajiwa kutoa manufaa yafuatayo;

Mosi,kuwakutanisha Wachimbaji na Wafanyabiashara kwa lengo la kuuza nakununua madini hivyo kuwapatia wachimbaji wadogo soko la uhakika lamadini wanayochimba.

Pili,kupitia masoko haya, Serikali inataraji wachimbaji wadogo watapatabei nzuri ya madini kutokana na uwepo wa wanunuzi wa uhakika kutokaNdani na Nje ya Nchi. Aidha, Tume ya madini itaratibu bei ya madinikwenye soko na kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata mapatowanayostahiki.

Tatu,Kuondoa tatizo la kupunjwa na kudhulumiwa kwa wachimbaji wadogo naWafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu. Udhibiti huoutafanyika kwa kuhakikisha vifaa vya kupimia uzito na ubora wa madinivinakuwepo na kutumika ipasavyo kwenye soko.

Nne,soko hili pia litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa nawajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana. 

Tano,Kuokoa muda na gharama nyingine katika kuendesha biashara ya madinikwa kuhakikisha huduma zote muhimu kwenye eneo moja (onestop center)kwa Wafanyabiashara ikiwemo huduma za Tume ya Madini, Mamlaka yaMapato Tanzania (TRA), Halmashauri na nyinginezo. 

Mwisho,Kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali na upatikanaji watakwimu za biashara ya madini. 


NduguWananchi,

Nimatumaini yangu kuwa soko hili litakuwa na tija kubwa hivyo tunawajibu wa kuhakikisha kuwa Soko hili linastawi na kuwanufaishawalengwa.

NduguWananchi,

Katikakuhakikisha soko hili linafikia malengo ya kuanzishwa kwake,tunaiomba Wizara ya Madini ishiriki kwenye maeneo yafuatayo:- 

Moja,Ishirikiane kwa karibu na Serikali ya Mkoa, kusimamia soko hilikikamilifu na kwa ufanisi ili lilete manufaa yanayokusudiwa. 

Pili,Kupitia Tume ya Madini ihakikishe inakamilisha ufungaji waMiundombinu na vifaa vyote muhimu na uwepo wa rasilimali watu yakutosha ili soko hili lifanye kazi kwa ufanisi. 

Tatu,Iendelee kushirikiana na wadau wote muhimu kuandaa utaratibu maalumwa kutoaelimukwa wachimbaji wadogo kuhusu namna soko linavyofanya kazi, faida zakena mambo mengine yatakayolitangaza soko hili kwa Mchimbaji naMfanyabiashara na hivyo kulitumia soko ipasavyo; 

Nne,Ihakikishe Viongozi na Watendaji wote wa Serikali wanasimamia kwaweledi, uaminifu na uadilifu, Sheria, Kanuni na miongozo ya Serikalikuhusu sekta hii ya madini kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wamadini. 

Tano,Watendaji wa Idara na Taasisi zote za Serikali zinazohusika na Sektaya Madini kuhakikisha wanaheshimu mipaka ya majukumu yao ilikulisimamia vizuri soko hili na kufanya kazi kama ilivyokusudiwa. 

Sita,Kushirikiana na Vyama na Mashirikisho ya Wachimbaji naWafanyabiashara wa madini kuandaa Mpango Kazi mahsusi kwa ajili yautekelezaji wa majukumu ya soko hili ili lisigeuke kuwa kikwazo kipyakwa Wachimbaji na Wafanyabishara wa madini. 

Saba,Vyombo vya Ulinzi na Usalama tutahakikisha vitoa ulinzi wa soko wakutosha katika soko hili muda wote, ili watendaji, malizitakazokuwemo, vitendea kazi na miundombinu yote iwe salama mudawote. 

Nane,Kuhakikisha maombi ya leseni za biashara na uchenjuaji wa madiniambayo hayajapatiwa leseni yanakidhi vigezo na kupatiwa leseni hizokwa wakati ili kila mdau anayehusika na biashara kwenye soko hiliatambulike kisheria.


NduguWananchi,

Kufuatiakuanzishwa kwa masoko haya niwasihi wadau wote wa madini kulitumiasoko hili na kuacha vitendo vya utoroshaji wa madini. Serikali kwaupande wake, haitomvumilia mtu yeyote yule atakaye jihusisha nautoroshaji wa madini. Nitoetahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa atakayekamatwa anatoroshamadini, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madiniatakayokuwa akiyatorosha.

NduguWananchi,

Kamamtakavyoona, lengo la Serikali kuanzisha masoko ya madini ni zuri nalina maslahi mapana ya nchi. Hivyo, ni vyema tuhakikishe kwa pamojatunayalinda masoko haya, tunayatetea na tunayawezesha kwa kadritunavyoweza. Kwa upande wa Serikali, itahakikisha masoko hayayanaendeshwa kwa njia shirikishi, uwazi na uadilifu ili sote kwapamoja tunufaike nayo. 

Mwisho,nimalizie kwa kuwashukuru wote kwa kufika kwenye shughuli hii muhimu,na kwa kuunga mkono jitihada hizi ambazo Mheshimiwa Rais wetuamezipigania na hatimaye leo tumezindua Soko la madini katika Mkoawetu wa Dodoma. Wote Hongereni sana. 


NduguWananchi, 

Baadaya kusema hayo, sasa nipo tayari kuzindua rasmi Soko la MadiniDodoma.

AHSANTENIKWA KUNISIKILIZA



Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.