• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MMMAM DODOMA WAFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI ROBO YA PILI 2024

Imetumwa : January 24th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Maafisa lishe na Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma, wamekutana leo Januari 24, 2025 kwenye ukumbi wa jengo la CCT Jijini Dodoma katika kikao kazi cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Malezi na Makuzi ya Mtoto (MMMAM) kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2024, unaotekelezwa katika Halmashauri zote nane za Mkoa huu.

Akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Afisa Afya upande wa Mazingira kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Seksheni ya Afya Bw. Nelson Rumbeli, amesema;

“Tunataka tutafsiri ni mikakati ipi imefanya vizuri kwenye Halmashauri fulani kuhusiana na huu utekelezaji. Tunahitaji tujiulize ni kwa jinsi gani imefanyika vizuri, imetekelezwa vipi na imefanya vizuri kwenye kundi gani. Nia hasa ni kuboresha na kuainisha changamoto tulizokutana nazo wakati wa utekelezaji wa Mpango huu”

Kadhalika, Diwani wa Halmashauri ya Chemba Mhe. Mwanaharusi Bakari Bato, amezungumzia suala la ushirikishwaji haba wa wadau kwenye mafunzo ya lishe yanapofanyika kwenye Halmashauri.

“NGO’s zilizopo kwenye Halmashauri zishirikishe ma-championi, sisi huwa tunatoa elimu bila kupata chochote, na tutaibua mengi ambayo yatakua faida kwenu. Mnapoleta taarifa zenu zinaboreka pia kuwashirikisha wahudumu wa afya kwenye mambo haya ya makuzi na malezi ni vizuri zaidi kwani watakwenda kuitoa kwa jamii”. Mhe. Bato

Aidha, Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Amina Mafita, amezungumzia ubainishaji wa awali wa watoto wenye ulemavu na kusema, anatamani kufahamu zoezi hilo limefikia hatua gani kwa sababu kuna vitengo maalumu ikiwemo shule jumuishi ambazo zina watoto hao hivyo nguvu kubwa inatakiwa kuelekezwa kwenye kuwabaini ili wapatiwe huduma muhimu.

Kikao hicho kilifungwa kwa kufikia maazimio mawili ambayo ni ufuatiliaji wa matukio ya ukeketaji kwa watoto wa kike yanayofanyika katika Halmashauri ya Chemba pamoja na kushirikisha makundi mengine ya wadau katika utendaji kazi ikiwemo ma-championi, viongozi wa dini na watu maarufu waliopo kwenye jamii zetu kwani wanachochea ustawi wa jamii.  


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu                               #mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.