• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MPANGO WA UPANDAJI MITI KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Imetumwa : June 1st, 2022

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, ambaye pia ndiye mgeni rasmi,ameshiriki katika zoezi la upandaji miti katika Mji wa Serikali wa Mtumba uliopo Mkoa wa Dodoma ikiwa ni katika harakati za kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya Mazingira Duniani June 05 Mwaka huu. Hafla hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kupanda miti ili kutimiza lengo la kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani ikiwa ni kutokana na asili ya ukame iliyopo katika Mkoa huu. Hivyo Serikali kupitia wadau na Taasisi mbalimbali zinazoshughulikia Mazingira, imeona ni vema ufanyike utaratibu wa kuufanya mji wa Dodoma ambao ndio makao makuu ya nchui kuwa na Miti ya kutosha.

Akitoka maelekezo mafupi ya uendelezaji wa Mji wa Serikali, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Bw. John Jingu, amesema Mji wa Mtumba unahusisha ujenzi wa majengo ya Taasisi za Kiserikali, Wizara na miundombinu ya barabara zenye urefu wa Km 51.2, ujenzi ambao umefikia asilimia 99 mpaka Sasa. Tayari ujenzi wa Ofisi 23 umekamilika na Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 300 ili kukamilisha majengo yaliyosalia. Kuna ujenzi wa Ofisi 24 ambao unaendelea ukiwa umefikia asilimia 28 mpaka 40 kukamilika, inatarajiwa kufikia mwezi Oktoba mwaka huu ujenzi utakuwa umekamilika.

Katika kutimiza azma ya Dodoma ya Kijani Wakala wa Uhifadhi wa misitu nchini, TFS, imedhamiria kupanda Miti 550,000 katika maeneo mbalimbali Mkoani Dodoma hadi kufikia Februari 2023. Ofisi ya Waziri Mkuu imeweka mkataba wa utekelezaji wa zoezi la upandaji miti ili kutimiza azma ya kuikijanisha Dodoma kama miji mingine Duniani.

Kamishna wa Uhifadhi wa Maliasili ikiwemo miti, Profesa. Dos Santos Silayo akitoka maelezo juu ya upandaji miti katika Mji wa Serikali Mtumba, maarufu kama "MAGUFULI GOVERNMENT CITY" ameeleza kuwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamo wa Rais mwaka 2017, alizindua mpango wa upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma. Lengo la mpango huo ni kupanda miti 5,075,000, katika kipindi cha miaka minNe. Jumla ya Miti 26,200 ndio iliyokwisha pandwa mpaka sasa katika Mji wa Dodoma. Prof. Dos Santos  ameongeza kuwa kutokana na upandaji miti unaendelea katika kipindi cha kiangazi, mpango mkakati uliopo ni kufunga mifumo ya umwagiliaji na kunyunyuza maji ili kuilinda Miti isikauke na hatimaye kufa. “Takribani Miti 550,000 itapandwa katika eneo hili ambayo itakua mchanganyiko wa matunda kama miparachichi, mipera, miembe, michungwa na milimao pamoja na upandaji wa miti ya vivuli hivyo tume ya umwagiliaji itafanya kazi kwa ukaribu sana kuhakikisha kuwa kufikia mwaka 2023, Mtumba inakua ya tofauti kwa upatikanaji wa matunda ya aina zote hizo”.Amesisitiza Prof. Silayo

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TARURA,Bw. Venant Komba ambaye ni Mkurugenzi wa Wakala wa Barbara za vijijini, TARURA Bw. Komba ameeleza kuwa barabara zenye urefu wa km 51.2,njia za waenda kwa miguu, mitaro ya Maji yenye urefu wa km 74 pamoja na nyongeza ya barabara zenye urefu wa km 7.9 zinatarajiwa  kukamilika. “Tunashirikiana kwa karibu na TFS kwa kutenga fedha na kushiri katika zoezi la kuufanya Mji wa Serikali kuwa kijani na wa kuvutia”.Amesema Bw.Komba

Mhe.Mary Masanja ambaye ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii  ameeleza kuwa, tunaadhimisha siku ya uhai wa Miti na kusisitiza kuwa Miti ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na jamii kwa ujumla, kwani Misitu inatoa asilimia 45 ya malighafi, hunyonya hewa ukaa na kutupatia hewa safi.Maisha ya mwanadamu hutegemea misitu tangu kuzaliwa hadi ukomo wa maisha yake hivyo tunatakiwa tuhakikishe misitu inakua salama wakati wote.

Akimkaribisha mgeni rasmi Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais- Mazingira Mhe. Suleiman Jafo alitoa historian fupi ya zoezi la upandaji miji  kwa kusema kuwa huu ni mwaka wa 50 kuadhimisha siku ya mazingira Duniani na kazi hii ilianzia kwenye eneo lenye heka 3000 la Iyumbu Park tarehe 28 Mei, 2022. Lengo ni kupanda Miti Milioni 276 kwa mwaka katika halmashauri zote  za Mkoa wa DODOMA.

Akihitimisha hafla hiyo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) amechagiza zaidi  kwa kusema asilimia 45 ya sekta ya Misitu inachangia upatikanaji wa  malighafi ya ujenzi , kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji  na hivyo kulinda mazingira. Misitu huchangia ongezeko la pato la Taifa na mtu mmoja mmoja. Waziri Mkuu amesisitiza kuwa suala la kupanda miti lipewe kipaumbeke na kila mmoja wetu."Tumeirithi na tuitunze miti hii kwa faida ya vizazi vijavyo. Hata mifugo na binadamu tunategemea miti kwa maisha. Kitendo cha kukata miti ni kujiumiza. Sisi wenyewe. Miti hutupatia kivuli, hewa safi na hupendezesha mazingira yetu." Mhe. Majaliwa

Waziri Mkuu alitoa Wito wa upandaji miti katikati ya barabara na pembezoni ili kutekeleza suala la uhifadhi wa mazingira.Aidha Mhe. Kasimi Majaliwa Majaliwa ametoa maagizo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwa kushirikiana na Taasisi ya TFS na TARURA kuhakikisha ujenzi wa miundo mbinu ya barabara unakamilika na kupanda miti maeneo yote .TFS na TARURA kutoa taariufa za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya ujenzi na miche hiyo.Wizara ya Fedha iwawezeshe . Taasisi zote za miundo mbinu kama vile TTCL, TEMESA, EGA na wengineo kuhakikisha taratibu za miundo mbinu zipo tayari na apate taarifa ifikapo 06/06/2022. Aidha Mhe. Waziri Mkuu ametaka wananchi waelimishwe  juu ya umuhimu wa mazingira na upandaji miti,pia amewataka Wataalam kuwekeza katika uzalishaji wa miche na mbegu bora.

Akizungumzia suala la Sensa Mhe. Waziri Mkuu amesisitiza wananchi wote kuhakikisha kuwa wanahesabiwa, "Hakikisheni nyumba zote zimepewa namba na anuani. Sensa ni muhimu Kila mtu ashiriki" amesisitiza .Mhe.Majaliwa. Aidha Waziri Mkuu amewahimiza wananchi wote ambao bado hawajachanja kuchanja kwani UVIKO-19 bado upo. Pia amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa awamu ya Sita kwa kuhamia Dodoma.

Ujenzi wa Mji wa Serikali wa Mtumba kama unavyojulikana kuwa 'MAGUFULI CITY' ulianza mwezi Novemba 2018 ambapo umepangwa kuhusisha maeneo ya Biashara, vituo vya magari ya abiria,hotel za kitalii, huduma za kibenki, maofisi, jengo la Cinema pamoja na majengo makubwa ya biashara. Pongezi na shukrani nyingi ziende kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha za Ujenzi wa awamu ya pili wa majengo 24 ya ghorofa, Ofisi za Mabalozi na jengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Pongezi kwa Wizara zote pamoja na Halmashauri ya jiji la Dodoma  kwa ujenzi wa hotel kubwa na ya kifaharil ambayo inaendelea kujengwa.

MWISHO.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.