• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"MWELEKEO WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA NI WANANCHI" rAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Imetumwa : November 27th, 2022

Mhe. Rais nikupongeze kwa kazi za kitaifa na kimataifa unazozifanya kwa manufaa ya Watanzania" Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa hadhala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pamoja na Wananchi wa Wilaya ya Chemba.

Akizungumza, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amewaeleza wananchi wa Chemba kuwa  mwelekeo wa Serikali ya awamu ya Sita ni wananchi ambapo msisitizo mkubwa ni kwenye elimu, maji, umeme,afya pamoja na kilimo.

Akizungumza miradi ambayo imefanywa na Serikali ya awamu ya sita katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Mkuu wa Mkoa wa  Dodoma,  Mhe. Rosemary Senyamule ametaja miradi mbalimbali ambayo Mhe. Rais ameifanya katika Halmashauri hiyo. Miradi hiyo ni pamoja na Elimu ambayo inahusisha ujenzi wavymba vya madarasa pamoja na mikopo ya vyuo vikuu, afya, kilimo, barabara pamoja na umeme.

Mhe.Senyamule amesema kuhusu sekta ya elimu,Mhe. Rais ametoa kiasi cha Tsh.9.7 bln, amejenga chuo cha VETA kwa gharama ya  Tsh. 2.2 bln na hivyo kwa mara ya kwanza Halmashauri ya Wilaya ya Chemba imepata chuo cha VETA. Aidha ujenzi wa vyumba vya  madarasa 46 unaendelea na madarasa hayo yatakamilika kabla ya mwezi Januari 2023 ili kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaingia madarasani. Aidha katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu wanaendelea na masomo Mhe. Rais ametoa Tsh.24.5bln ikiwa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

"Kwa Upande wa Sekta ya afya Mhe Rais ametoa Tsh. 3.3 bln na bado kuna mradi wa kimkakati wa hospital ya Wilaya ambayo ujenzi wake bado unaendelea kwa gharama ya Tsh.2.0 bln" RC Senyamule.

Mhe. Senyamule amesema kuwa Uchumi wa  Wilaya ya Chemba unategemea sana Kilimo na Ufugaji.Kwa kuwajali wananchi wa Chemba Mhe. Rais ametoa Tsh. 1.0 Bln kwa ajili ya ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao ambalo ujenzi wake umekamilika.Hali kadhakila Mhe.Rais kwa kuwajali wakulima ametoa mbegu na mbolea za ruzuku pamoja,kwa kuwajali wafugaji Mhe. Eais ametoa fedha ambazo  zimewezesha ujenzi wa Majosho ya kuogeshea wanyama.

Aidha katika kukabiliana na kupanda kwa bei za vyakula Mhe. Senyamule amemueleza Mhe. Rais kuwa kuanzia wiki ijayo wananchi wa Chemba wameahidiwa kupata vyakula kwa bei rahisi.

"Kuhusu sekta ya maji, upatikanaji wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ni 32%, hata hivyo kuna miradi 11 ya maji ambapo ikikamilika itapunguza changamoto hiyo, kwani itaongeza upatikanani wa maji kufikia 55%. Pamoja na miradi hiyo 11 ujenzi wa bwawa la Farkwa ambalo Serikali ya awamu ya sita chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan umetoa jumla ya Tsh. 300 bln, mradi huu utatatua changamoto ya maji katika Halmashauri za Bahi, Chemba, Chamwino, Kondoa pamoja na Jiji la Dodoma.

Akizungumzia barabara Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imetoka kiasi cha Tsh. 3.3 trilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Halmashauri ya Chemba. Pamoja na hayo Serikali ya awamu ya sita imetoa kiasi cha Tsh. 30 bln kuhakikisha kila nyumba katika Halmashauri ya Chemba inapata umeme.

MWISHO.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.