• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI ZAIDI YA BILION 16

Imetumwa : September 30th, 2023


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Ally Senga Gugu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba.

Makabidhiano hayo ya Mwenge wa Uhuru 2023 yamefanyika leo tarehe 29 Septemba 2023 katika Viwanja vya Bahi - Sokoni Wilayani Bahi Mkoani Dodoma.

Akipokea mwenge huo Bw. Gugu amesema kuwa lengo kubwa la kuupokea mwenge ni kufanya uchechemuzi wa miradi pamoja kuhamasisha upendo, amani na ushirikiano.

Katibu Tawala huyo akizungumza muda mfupi baada ya kupokea mwenge huo wa Uhuru amesema kuwa utapita katika Wilaya zote saba (7) na Halmashauri nane (8) zikiwemo Bahi, Chemba, Kondoa Dc, Kondoa Mji, Dodoma jiji, Chamwino, Mpwapwa na kumaliza ratiba kwenye Wilaya ya Kongwa.

Amesema mwenge huo wa Uhuru utakimbizwa kwa kilometa elfu moja Mia nane na tini na tatu (1893) na katika mbio zake utapitia jumla ya Miradi arobaini na tano (45) ambapo miradi kumi na tano (15) itawekewa mawe ya msingi na miradi kumi na tisa (19) inatarajiwa kuzinduliwa na kumi na moja (11) itatembelewa yenye jumla ya thamani zaidi ya Billioni 16. ikiwepo miradi ya sekta ya elimu,afya miradi ya utunzaji wa Mazingira.

Aidha, Bw. Gugu amesema kuwa miradi hiyo ambayo itazinduliwa na mbio za Mwenge wa uhuru italenga kuwasaidia watanzania hususan wakazi wa maeneo husika.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga akitoa taarifa za mwenge katika Mkoa wa Singida kabla ya makabidhiano amesema umefanikiwa kuzindua miradi mbalimbali na mingine kuwekwa mawe ya msingi.

Amebainisha miradi ambayo imetekelezwa katika Mkoa wa Singida na Wilaya zake ni pamoja na sekta ya Elimu, Afya, Utawala, Kilimo, Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Barabara, Nishati na Maji.

Akizungumzia miradi amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Septemba 2023 miradi yenye thamani ya fedha kiasi shillingi Bilioni 224 imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Dkt.Mganga amesema sekta ya Elimu amesema kuwa Jumla ya sh.Bilioni 34.08 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya elimu hususani ujenzi wa shule mpya za BOOST na shule mpya za sekondari kupitia mradi wa SEQUIP pamoja na utoaji wa elimu bila malipo kutoka shule ya msingi hadi kidato cha nne.

Nae, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa Bw.Abdalla Shaib Kaim amesema kuwa lengo la kukagua miradi hiyo ni kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaendana na thamani ya fedha.

Amesema serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hasani,imekuwa ikipambana kutafuta fedha kwa kwa ajili ya maendeleo hivyo ni jukumu la watendaji kuhakikisha wanasimamia miradi kwa thamani ya fedha inayotakiwa.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.