• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"Nimedhamiria Kumaliza Migogoro ya Ardhi Baina ya Wakulima na Wafugaji" RC-SENYANMULE

Imetumwa : September 10th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule, ametoa kauli hiyo alipokua akizungumza na wafugaji kutoka Halmashauri  zote za Mkoa wa Dodoma, kwenye kikao alichokiitisha kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya ufugaji.

Mhe. Senyamule, alianza kwa kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wafugaji ambapo kero iliyoonekana kuwa kubwa zaidi ni migogoro ya ardhi baina ya Wakulima na Wafugaji, uhaba wa maeneo ya malisho, majosho, soko la uhakika la nyama na bidhaa nyingine za mifungo hasa nje ya nchi.

Baada ya kusikiliza kero hizo, Mhe. Senyamule akaja na maelekezo kwa Idara ya ardhi kuhakikisha inajipanga na kuwasilisha mezani kwake mpango Mkakati wa utatuzi wa migogoro ya ardhi ndani ya kipindi cha wiki moja huku wafugaji ambao wapo tayari kupimiwa maeneo yao, zoezi lifanyike tena kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

"Sekta ya ardhi, naagiza mukae na kuja na majawabu ya lini maeneo ya wafugaji yatapimwa tena kwa gharama nafuu kwani Serikali tutalisimamia hili na kuhakikisha maeneo yote yanapimwa. Nimedhamiria kumaliza migogoro ya ardhi ndani ya Mkoa wa Dodoma"  Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Hata hivyo, Mhe. Mkuu wa Mkoa, ameongeza kuwa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ana matamanio makubwa ya kuiinua sekta ya Kilimo na ufugaji kutokana na jitahidi anazozifanya ikiwemo kuanzishwa kwa miradi mingi inayozingatia mahitaji ya Wakulima na Wafugaji kwani fedha nyingi zimetoka kuwezesha idara ya kilimo na ufugaji. Rais pia ametafuta masoko kwa ajili ya nyama ya Tanzania iuzike nje ya nchi, viwanda vikubwa vinatarajiwa kuanzishwa kama vile kiwanda cha Nyama, maziwa na ngozi ambavyo tayari maeneo yametengwa kwenye Wilaya za Bahi, Mpwapwa na Chamwino huku zikitengwa Shilingi Bilioni 7 kwa ajili ya miradi hiyo.

Akiwasilisha taarifa fupi ya sekta ya kilimo Mkoa wa Dodoma, Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji Mkoa Bi Aziza Mumba amesema, Mkoa una hazina kubwa za aina mbalimbali za mifugo ambapo takribani asilimia 99 ya mifugo iliyopo ni ya asili. Mkoa unakadiriwa kuwa na mifugo 5,432,005 ikijumuisha Ng'ombe 1,823,715, Mbuzi 909,073, Punda 27,994, Kondoo 23,096, Nguruwe 110,189, Kuku 2,095,660 na Bata 142,278. Halmashauri ya Chamwino inaongoza kwa idadi ya mifugo ikifuatiwa na Chemba, Mpwapwa na Bahi.

"Eneo linalofaa kwa ufugaji ni Hekta 1,215,758 ambayo ni sawa na asilimia 29.43 ya eneo lote la Mkoa wa Dodoma (Hekta). Kati ya maeneo yote yaliyotengwa ni eneo moja la Ranchi ya Kongwa linalomilikiwa na Serikali na ndilo limeendelezwa" Amesema Bi Mumba.

Naye Meneja wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Dodoma Bwana Sostenes Kibwengo, amewasihi wafugaji kukemea vitendo vya Rushwa na kutokukubali kununua haki yao. Amesema kuwa, anayetoa fedha kununua haki yake na anayepokea fedha hiyo wote wanatenda makosa kwa mujibu wa Sheria ya Kupambana na Rushwa. Bw.Kibwengo amewataka wafugaji kupiga namba ya dharura ambayo ni 113 watoe taarifa endapo watakutana na mazingira ya kuhitajika kutoa rushwa.

Mwenyekiti wa Chama Cha wafugaji Tanzania Jeremiah Wambura, amewaasa wafugaji kufuata Sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali katika sekta ya ufugaji ikiwemo kuweka hereni kwenye mifugo yote nchini, kwani hii inasaidia utambuzi wa mifugo. Utambuzi wa mifugo umetajwa kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM hivyo ametoa agizo kwa Katibu wa chama cha Wafugaji  Wilaya ya Chemba kumsimamisha Kiongozi wa Chemba ambaye anatuhumiwa kupingana na maagizo ya Serikali juu ya zoezi la utambuzi wa mifugo kwani Taasisi yoyote haitakiwi kupingana na Serikali bali kama kuna tatizo, anapaswa kuliandika na kupeleka malalamiko yake kwenye Mamlaka husika.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.