• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

PROF. MWAMFUPE: MAONESHO YA NANE NANE YAWASAIDIE WAKULIMA NA WAFUGAJI WETU KUONGEZA TIJA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA UZALISHAJI

Imetumwa : August 6th, 2017

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma Mheshimiwa Profesa Davis Mwamfupe amesema bado Maonesho ya Kilimo na Mifugo (Nane Nane) Kanda ya Kati hayajafanikiwa kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi wetu kwa kiasi kinachoridhisha kuwawezesha kubadili shughuli zao na kuzifanya kuwa na tija inayoridhisha.

Amesema Maonesho ya Nane Nane yamekuwepo kwa miaka mingi maeneo mbalimbali ya nchi katika Kanda mbalimbali na ukiyatembelea utakutana na vitu vya kuvutia sana hususani Teknolojia na mbinu bora za uzalishaji kilimo na mifugo ambazo zinauwezo wa kuleta tija kubwa lakini bado changamoto kubwa mambo yote bora na mazuri yanayopatikana kwenye Maonesho bado hayajaweza kumfikia mkulima kwenye ngazi za msingi, akitoa mfano kuwa unaweza kutoka umbali usiozidi kilomita mbili (2) kutoka kituo (Uwanja) cha Maoneshocha Nzuguni kilipo utashangaa kukuta mkulima analima kilimo cha kienyeji ambacho hakina manufaa.

Profesa Mwamfupe aliyasema hayo Agosti 6, 2017 wakati alipofanya ziara kutembelea Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Maonesho vya Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

“Teknolojia inayooneshwa kwenye Maonesho haya bado haijaweza kuwafikia wakulima na wafugaji wetu kwenye vijiji vyao wanapoendeshea shughuli zao za kilimo na mifugo” alisema Profesa Mwamfupe. Aliongeza kuwa bado teknolojia na ubunifu unaopatikana kwenye Maonesho haya unahitaji kuwafikia wakulima wa chini kabisa.

Alitoa wito kwa Mamlaka zinazohusika kuhakikisha Kiwanja cha Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati Nzuguni kinakuwa kituo cha Shamba Darasa la kilimo mifugo na uvuvi cha kudumu na wakati wote wataalamu wa kilimo na mifugo wawepo kituoni hapo kipindi chote cha mwaka wakisimamia shughuli za kilimo na mifugo kituoni hapo na Halmashauri za Wilaya zilete Wakulima na Wafugaji wao kujifunza na kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za uzalishaji .

Amezitaka sasa Halmashauri za Wilaya Kanda ya kati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaounga mkono shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi waone namna wanavyoweza kuifikisha kwa wakulima na wafugaji wetu elimu inayopatikana kwenye Uwanja wa Maonesho Nzuguni. Aidha, amewataka wananchi wa Mikoa ya Dodoma na Singida hususani wakulima, wafugaji na wavuvi kutembelea Maonesho hayo kwa wingi kwa kuwa mambo mazuri yakujifunza yapo mengi kubwa likiwa jinsi Teknolojia na mbinu bora za kuongeza tija ya uzalishaji mazao ya kilimo na mifugo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.