• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Imetumwa : April 21st, 2018

Mkoa wa Dodoma Makao Makuu ya nchi unatarajia kupokea Ugeni Mkubwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli anayetarajiwa kuwasili Dodoma Siku ya Jumapili Aprili 22, 2018 kwa shughuli mbalimbali za kiserikali.

Akitoa taaarifa kwa Umma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema kuwa akiwa hapa Mkoani Dodoma, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Aprili 26, 2018 atakuwa Mgeni Rasmi kwenye sherehe za Maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika katika Uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 12:00 alfajiri.

Dkt. Mahenge pia amesema Aprili 27, 2018 Mhe. Rais Magufuli atazindua Barabara ya Dodoma – Babati (Bonga) yenye urefu wa Km 231.8, Sherehe za uzinduzi wa barabara hii zitafanyika kwenye Wilaya ya Kondoa Eneo la Bicha.

Taarifa hiyo ya Mkuu wa Mkoa imeeleza kuwa Mhe. Rais atazindua Jengo jipya la PSPF na Tawi jipya la Bank ya NMB Kambarage lililopo mtaa wa barabara ya Chimwaga Aprili 23, 2018 na pia atalihutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambalo awamu hii linafanyika hapa Nchini Tanzania Mkoani Dodoma Siku ya Jumanne Aprili 24, 2018.

Dkt. Mahenge amesema tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atangaze azma yake ya kuhamishia Serikali Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Nchi hapo mnamo Julai 23, 2016 na hatua zote zilizofanyika hadi sasa ikiwemo Wizara zote kuhamia Mkoani Dodoma, Serikali imekuwa ikiupa Mkoa wa Dodoma heshima na hadhi ya Kipekee ya Makao Makuu kwa Kuelekeza Shughuli nyingi na nyeti za Kitaifa kufanyikia hapa Dodoma.

Ametoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na hata Mikoa ya jirani, kuenzi heshima hii kubwa kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kwenye Sherehe za Maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye Uwanja wa Jamhuri na sherehe za uzinduzi wa Jengo jipya la PSPF na tawi jipya la Benki ya NMB.

Aidha, kwa wananchi wa Kondoa na maeneo jirani amewasisitiza wajitokeze kwa Wingi kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa barabara ya Dodoma Babati (Bonga) Km 231.8 ambayo ni kichocheo kikubwa cha shughuli za uzalishaji na uchumi wa ukanda wote wa Bahi, Chamwino, Chemba na Kondoa

“Nisisitize kuwa barabara hii ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini ( Great North Road) inayoanzia Cape Town Afrika Kusini hadi Cairo Misri hivyo ina umuhimu wa kipekee kwetu wananchi wa Dodoma kwa upande wa shughuli za uzalishaji viwanda na uchumi”

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • ZAIDI YA BILIONI 11 ZILIVYOWANUFAISHA WANUFAIKA WA TASAF DODOMA

    May 15, 2025
  • DODOMA NA MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’

    May 14, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WASISITIZWA KUHUBIRI AMANI

    May 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.