• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DOM DKT. MAHENGE AZINDUA MKAKATI WA MIAKA MITANO (2018 - 2022) WA MAENDELEO YA MNYORORO WA THAMANI WA ZAO LA ALIZETI MKOANI DODOMA (HABARI KATIKA PICHA)

Imetumwa : November 18th, 2018

Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikata utepe kuzindua kitabu cha Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa Zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma, kulia ni katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Kessy Maduka na kushoto ni katibu Tawala Msaidizi anaesimamia Sekta za Uchumi na Uzalishaji Mkoani Dodoma Bi. Aziza Mumba. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi. 


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akiwaonesha wadau wa Alizeti (hawapo pichani) kitabu cha Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma wakati alipouzindua, kulia ni katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Kessy Maduka na kushoto ni katibu Tawala Msaidizi anaesimamia Sekta za Uchumi na Uzalishaji Mkoani Dodoma Bi. Aziza Mumba. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Veneranda Makotta kitabu cha Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya kuuzindua mkakati huo, Dkt. Mahenge aliwakabidhi Mkakati huo wakuu wote wa Wilaya, Wenyeviti Wote wa Halmashauri, Wakurugenzi wote wa Halmashauri, Maafisa kilimo wote wa Wilaya Mkoani Dodoma na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Alizeti Mkoani Dodoma ili wakasimamie utekelezaji wa mkakati huo. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga kitabu cha Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya kuuzindua mkakati huo, Dkt. Mahenge aliwakabidhi Mkakati huo wakuu wote wa Wilaya, Wenyeviti Wote wa Halmashauri, Wakurugenzi wote wa Halmashauri, Maafisa kilimo wote wa Wilaya Mkoani Dodoma na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Alizeti Mkoani Dodoma ili wakasimamie utekelezaji wa mkakati huo. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Mukunda kitabu cha Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya kuuzindua mkakati huo, Dkt. Mahenge aliwakabidhi Mkakati huo wakuu wote wa Wilaya, Wenyeviti Wote wa Halmashauri, Wakurugenzi wote wa Halmashauri, Maafisa kilimo wote wa Wilaya Mkoani Dodoma na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Alizeti Mkoani Dodoma ili wakasimamie utekelezaji wa mkakati huo. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri kitabu cha Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya kuuzindua mkakati huo, Dkt. Mahenge aliwakabidhi Mkakati huo wakuu wote wa Wilaya, Wenyeviti Wote wa Halmashauri, Wakurugenzi wote wa Halmashauri, Maafisa kilimo wote wa Wilaya Mkoani Dodoma na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Alizeti Mkoani Dodoma ili wakasimamie utekelezaji wa mkakati huo. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkakati huo wa miaka mitano 2018 - 2022 wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma ulikabidhiwa pia kwa wakulima, viongozi wa vikundi vya wakulima, maafisa kilimo na ugani na wadau muhimu wa kilimo kama wanahabari.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga mashine ya kupandia Alizeti kitaalamu, mashine hizo zimetolewa na shirika la Dalberg ambalo ni moja ya wadau muhimu wa maendeleo ya sekta kilimo cha Alizeti Mkoani Dodoma, jumla ya mashine 24 ziligawiwa kwa Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya vikundi vya wakulima. Makabidhiano ya mashine hizo yalifanyika mjini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akikagua mashine za kisasa na za teknolojia rahisi za kupandia Alizeti wakati wa kukagua maonesho ya wadau wa maendeleo ya sekta ya Alizeti mkoani Dodoma yaliyofanyika sambamba na hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma. Mkakati huo wa miaka mitano (2018 - 2022) umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua mafuta ya alizeti yanayosindikwa na wanachama wa chama cha wakamuaji na wasindikaji mafuta ya alizeti Mkoani Dodoma (CEZOSOPA) wakati akitembelea maonesho ya wadau wa sekta ya alizeti mkoani Dodoma yaliyofanyika sambamba na hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa tatu kutoka kushoto) akikagua mbegu bora ya Alizeti aina ya “Record’ iliyoboreshwa ambayo inazalishwa hapahapa nchini na wataalamu wazawa na ambayo imeonesha tija kubwa katika mavuno ukilinganisha na mbegu zinazoingizwa kutoka nje ya nchi, Mhe. Dkt. Mahenge alikuwa akikagua maonesho ya wadau wa maendeleo ya sekta ya Alizeti mkoani Dodoma yaliyofanyika sambamba na hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma. Mkakati huo wa miaka mitano (2018 - 2022) umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na viongozi mbalimbali wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma wakipatiwa maelezo ya kitaalamu juu ya machapisho yanayotoa elimu ya kilimo bora cha Alizeti wakati wa maonesho ya wadau wa maendeleo ya sekta ya Alizeti mkoani Dodoma yaliyofanyika sambamba na hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma. Mkakati huo wa miaka mitano (2018 - 2022) umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akipata maelezo ya kitaalamu juu ya kilimo bora cha Alizeti kutoka kwa Mshauri wa kilimo wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Bernard Abraham wakati akikagua maonesho ya wadau wa maendeleo ya sekta ya Alizeti mkoani Dodoma yaliyofanyika sambamba na hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma. Mkakati huo wa miaka mitano (2018 - 2022) umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.


Picha ya pamoja kati ya Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na Wadau wa Sekta ya Alizeti Mkoa wa Dodoma mara baada ya uzinduzi wa Mkakati wa Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani wa Zao la Alizeti kwa Mkoa wa Dodoma. Mkakati huo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi. 

(PICHA NA HABARI ZOTE NA OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA) 

Mkoa wa Dodoma umezindua Mkakati wa miaka mitano (2018 - 2022) wa Maendeleo ya sekta ya kilimo cha Zao la Alizeti ambao unalenga kukuza mnyororo mzima wa thamani wa zao hilo na kuongeza tija ya uzalishaji kiwango kikubwa cha mbegu bora na kuongeza kiwango cha uzalishaji mafuta na hivyo kusaidia kupunguza kiasi cha mafuta yanayoingizwa kutoka nje ya nchi.

Mkakati huo umeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma na Wilaya zake zote saba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mnyororo mzima wa thamani wa zao hilo kwenye Mkoa wa Dodoma ambapo umelenga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kinara wa uzalishaji zao la Alizeti, pia kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti na kuiwezesha nchi kupunguza kiwango cha uagizaji mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge mara baada ya kuuzindua Mkakati huo wa miaka mitano ameukabidhi kwa Wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma, Wenyeviti Wote wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Dodoma, Maafisa kilimo na Wagani wote wa Wilaya Mkoani Dodoma, Wawakilishi wa Vikundi vya Wakulima na Wadau mbalimbali wanaofadhili Sekta ya Kilimo cha Alizeti Mkoani Dodoma na kuwataka waende wakausimamie utekelezaji wake.

Dkt. Mahenge amebainisha kuwa changamoto kubwa iliyopo sasa ni tija ndogo kwenye uzalishaji wa Alizeti inayochangiwa na ukosefu wa ujuzi katika uzalishaji pasipo kuzingatia kanuni bora za uzalishaji, ukosefu wa mitaji, ubovu wa miundombinu muhimu kama barabara, ukosefu wa nishati ya uhakika na uwekezaji mdogo katika sekta ya kilimo na kubainisha kuwa Mkakati huo umezingatia changamoto zote hizo.

Mkakati huo uliozinduliwa unalitambua zao la Alizeti kama zao la kipaumbele Mkoani Dodoma likiungana na Mazao mengine ya kipaumbele kama vile Zabibu, Korosho, pamba na mazao ya chakula yanayostawi vizuri Dodoma. Mkakati umetambua na kuainisha majukumu ya kila mdau kwenye mnyororo wa thamani wa zao la Alizeti na kuweka mfumo wa usimamizi wa utekelezaji.

Aidha, Mkakati umeainisha kuwajengea uwezo wakulima wa alizeti, wakamuaji mafuta ya Alizeti na namna ya kuongeza tija ya uzalishaji kutoka kg. 350 kwa Ekari na kufikia kg. 1000 kwa ekari ifikapo mwaka 2020. Mkakati pia umeeleza hatua za kuchukua ili kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi, ukulima mkubwa na uwekezaji mpya.


























































































Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.