• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DOM DKT. MAHENGE: TUMEWATENGUA VYEO WOTE WALIOHUSIKA NA UDANGANYIFU KWENYE MTIHANI WA DARASA LA SABA, ATAKAYETHUBUTU KUFANYA VITENDO KAMA HIVI KWENYE MTIHANI WA MARUDIO KUKIONA CHA MOTO

Imetumwa : October 3rd, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema kuwa uongozi wa Serikali Mkoa wa Dodoma umewavua madaraka waratibu Elimu ngazi ya kata watano (5) na Walimu Wakuu wa shule za msingi watano (5) kwenye Wilaya ya Chemba na Kondoa Mji waliobainika wazi wazi katika hatua za awali za uchunguzi kujihusisha na njama za udanganyifu wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (darasa la saba) kwa mwaka huu 2018.

Amesema kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI wametengua teuzi za uongozi wa idara ya Elimu ngazi ya Wilaya waliohusika katika kufanya udanganyifu huo, ambapo Afisa elimu wa Chemba na Afisa Taaluma wa Wilaya Chemba na Afisa elimu msingi wa Wilaya ya kondoa DC (Majina tunayahifadhi kwa sababu za kiuchunguzi) vyeo vyao vimetenguliwa.

Dkt. Mahenge amesema kuwa tukio la udanganyifu katika mtihani lililowahusisha waratibu hao wa elimu kata na walimu wakuu limesababisha baadhi ya Wilaya na shule katika Mkoa wa Dodoma kufutiwa mtihani na matokeo ya kuhitimu Darasa la Saba 2018 ambapo Halmashauri ya Mji Kondoa Shule moja ya Kondoa Integrity imefutiwa mtihani na matokeo na Halmashauri nzima ya Wilaya ya Chemba matokeo ya shule zote za msingi yamefutwa.

Amebainisha hayo Oktoba 3, 2018 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema Binafsi kwa niaba ya uongozi wote wa Mkoa ana masikitiko makubwa kwa tukio hili na vitendo vyote vilivyo nyuma yake na kuwa Athari za tukio hili ni kubwa kuanzia kwa watoto wenyewe, familia zao na pia limetia doa juhudi za Mkoa wa Dodoma kuinua kiwango cha Elimu na ufaulu. Aidha limesababishia Serikali hasara kubwa kwa kuingia gharama za kurudia mtihani kwa maana ya muda na nguvu kazi.

Ameongeza kuwa kufuatia kudanganyifu huo kwenye mtihani, Walimu wanne waliookuwa wasimamizi wa mitihani katika shule binafisi ya Kondoa Integrity nao wamesimishwa kazi kupisha uchunguzi na ameziagiza mamlaka za nidhamu kuwafungulia mashtaka wale wote waliohusika na tukio hilo na kutaka uchunguzi wa kina uendelee kufanyika ili kila yeyote atakayebainika kuhusika katika tukio hili achukuliwe hatua stahiki.

Ametanabaisha kuwa Kamati ya Mitihani ya Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Kessy Maduka imetekeleza wajibu wake wa kupokea, kulinda na kugawa mitihani kwa uadilifu mkubwa sana. Imekuwa karibu sana kufuatilia tukio hili la udanganyifu wa mitihani katika hatua zote na kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika.

Katika hatua nyingine Dkt. Mahenge ameipongeza Serikali kwa huruma iliyotoa ya kufuta matokeo lakini pia kuwaruhusu watoto kurudia mtihani. “Kwa uzito wa jambo hili na kwa lengo la kuzuia suala kama hili kutokea tena, tayari Serikali imechukua hatua stahiki kwa wale wote waliokula njama hizi” Ameongeza Dkt. Mahenge

Amewataka wale watakaopewa jukumu la kusimamia mtihani wa marudio kuhakikisha wanasimamia kwa ukamilifu mtihani wamarudio na kuhakikisha kuwa dosari zilizojitokeza hapo awali hazijitokezi tena na kuwa Serikali haina mzaha atakayethubutu kufanya vitendo hivi mkoani Dodoma atapata taabu sana.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.