• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AKABIDHI MAGARI KWA WAKUU WA WILAYA ZA BAHI;CHAMWINO.NA KONGWA

Imetumwa : March 24th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa magari matatu mapya kwa Wakuu wa Wilaya za Bahi, Chamwino na Kongwa ambayo yatawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa urahisi ikiwemo kuwafikia Wananchi, kusikiliza na kutatua kero zao.


Akikabidhi magari hayo kwa Viongozi hao wa Wilaya, Machi 24, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema;


“Mhe. Rais ametoa uzito kwa majukumu makubwa ambayo Wakuu wa Wilaya wanayafanya, na kwa kujali pia Watanzania ili waweze kuhudumiwa. Ametoa tena magari haya matatu ya kisasa kabisa ambayo yatawafanya Viongozi hawa kuwakimbilia Wananchi kwa haraka zaidi kwani kazi zao ni za dharura na zinataka vitendea kazi imara na vya uhakika”


Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, amesema Mhe. Rais katika bajeti ya 2024/2025, aliridhia kuendelea kununua magari kwa Wakuu wa Wilaya waliohitaji, hivyo Wakuu wa Wilaya watatu walipata magari mapya na mwaka huu Wakuu wa wilaya wanne watapata magari mapya.


Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya waliopokea magari hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S. Mayeka, amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa namna ambavyo ameitendea Wilaya yake kwa kuipatia gari jipya na amemuahidi kulitumia kwa kuwahudumia Wananchi wake kwani ataweza kuvifikia vijijiji vyote 87 na vitongoji 385 kusikiliza na kutatua kero zao.


Kadhalika, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi na MNEC  Bw. Donald Mejitii, amemshukuru Mhe. Rais kwa kuleta usafiri kwa Wakuu wa Wilaya kwani wao ndio wanaosimamia maendeleo na usalama kwenye Wilaya na wanamsaidia Mhe. Rais kwenye maeneo yao hivyo kwa usafiri huo, wanakwenda kutekeleza kasi ya ilani, usimamizi wa usalama na utulivu.





#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.