• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE APOKEA MABALOZI WANNE KUELEKEA ‘DIPLOMATIC CAPITAL TOUR ‘MEI 27

Imetumwa : May 26th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Mei 26, 2025 amepokea ugeni wa Waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania ambazo ni Sweden, Denmark, Finland na Norway waliofika ofisini kwake Jijini Dodoma kufuatia tukio la ziara ya Mabalozi lililoandaliwa na Mkoa huu linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumanne Mei 27.

Mabalozi hao wamefika Ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha na pia kupata taarifa za uwekezaji sambamba na vivutio vilivyopo Mkoani hapa kutokana na kushindwa kushiriki ziara iliyoandaliwa hapo kesho.

Akizungumza na Mabalozi hao, Mkuu wa Mkoa amewaeleza dhumuni hasa la kuandaa ziara hiyo;

“Wakati huu tumewaalika mje tuwaambie na kuwaonesha nini tunacho hapa Dodoma. Hatuwezi kutembelea sehemu zote kwa siku moja lakini nyinyi mnaweza kushawishi nchi zenu kuhamia Dodoma kwani Mihimili Mitatu ya Serikali yote ipo Dodoma hivyo ni wakati sasa wa kufikiria kuhusu uchumi wa Dodoma kwani Serikali imewekeza fedha nyingi kujenga miundombinu hapa.”

Kadhalika, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko ametumia wasaa huo kuelezea juu ya Mradi unaotarajiwa kutekelezwa Hombolo kwa kuufanya kuwa Mji wa Kidiplomasia kutokana na uwepo wa Ziwa Hombolo ambalo lipo umbali wa Km 70 kutoka Dodoma Mjini na eneo hilo ni la kimkakati kwani lipo karibu na Mji wa Serikali, eneo la Mabalozi pia kiwanja cha ndege cha  Msalato.

Ziara ya Mabalozi Jijini Dodoma imeandaliwa kwa kutambua mchango wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejenga mahusiano mazuri na nchi zote Duniani zinazowafanya wafurahie kuja Tanzania na haya yote wamekua wakiyafanya katika nchi mbalimbali hivyo sasa ni zamu ya Dodoma inakwenda na kauili mbiu ya “Dodoma Tupo Tayari kwa Ajili Yenu”


#dodomawearereadyforyou

#takedodomatotheworldandbringtheworldtododoma

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.