• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AWATAKA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA ITIFAKI YA DIPLOMASIA NA USTAARABU KUWA CHACHU KWA WENGINE

Imetumwa : January 26th, 2025

Na Sofia Remmi.

Dodoma-Habari Rs

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule amewataka Washiriki wa Mafunzo ya Itifaki ya Diplomasia na ustaarabu kupeleka elimu waliyoupata kwa wengine,na kwamba kwa kufanya hivyo elimu hiyo itakuwa na manufaa,kwani itawafanya watu wengi kubadilika.

Mhe. Senyamule ameyasema hayo leo Januari 26,2025 wakati akifunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku tatu ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Protocal Service Team ambapo jumla ya washiriki 110 kutoka katika mikoa 19 wamepata mafunzo.

"Nimefurahi kuona kundi hili kubwa linakwenda kuwa chachu kwa wengine.Nilikuwa nimekaa hapa natafakari hivi hawa watu 110,kila mmoja akienda kutoa elimu hii kwa watu 10 tu,maana yake elimu hii itakuwa imewafikia watu 1,100,hao si watu wachache,bali ni wengi sana".

Sambamba na kuwataka Washiriki hao kupeleka elimu hiyo kwa wengine,Mhe Senyamule amewataka  kuifanyia kazi  kwa wao wenyewe kubadilika.

" Kubadilika kunataka dhamira ya dhati ya kuchukua hatua,maadam mmejifunza,maneno yenu,matendo yenu yaoneshe kwamba ninyi ni watu wapya.

Tunayo kazi ya kufanya sisi wenyewe ambao tumepata mafunzo kuchukua hatua ya kubadilika.Lakini tunayo kazi kubwa ya kupeleka elimu hii kwa watu wengine,tusibaki nayo wenyewe.Watu wanafikiri kwamba ustaarabu unatokea tu,ustaarabu mtu anafundishwa.Amesema Mhe. Senyamule.

Kadhalika Mhe Senyamule amesema amefurahi kwamba Washiriki hao wamejifunza  Itifaki ya Mwenge wa Uhuru kwani watakuwa wameelewa maana na umuhimu wa Mwenge wa Uhuru,na kwamba watawaelimisha na wengine.

"Hapa kwenye  kujifunza kuhusu Mwenge kilichonifurahisha, ninyi sasa mmeshajua nini maana ya Mwenge wa Uhuru.Watanzania wengi hawajui,wengine wanasema Mwenge hauna sababu,ukawekwe makumbusho,lakini ninyi mtatusaidia kusema,kwa sababu mmeelewa," Mhe. Senyamule

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Taasisi ya 'Protocal and Services Team' (PST) Hussein Abubakari amesema wamepata mafanikio makubwa kwani mafunzo ya awamu hii yamekuwa na washiriki wengi tofauti na awamu iliyopita,huku  akiahidi kuwa taasisi yake itaendelea  kuratibu mafunzo hayo ili watu wengi zaidi wapate nafasi ya kujifunza.

Sambamba na kueleza mafanikio, Mkurugenzi huyo ameshukuru kwa ushirikiano ambao PST wamekuwa wakiupata kutoka kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Naye,Mkufunzi Mkuu  wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Dkt. Godwin Amani Gonde amesema kuwa washiriki hao wamejifunza dhana ya  Mwenge,Itifaki ya Mwenge, maana ya itifaki ,umuhimu wa itifaki katika maeneo ya kazi,Sheria za itifaki,Itifaki ya Mawasiliano,namna ya kuzungumza kama Watumishi wa Umma,Uvaaji,namna ya kula pamoja na falsafa ya utu na Utanzania.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo,Mchungaji Kelvin Mlingo amesema elimu waliyoipata watakwenda kuifanyia kazi kwa vitendo.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.