• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YABORESHA MAZINGIRA YA UTOAJI HUDUMA ZA MAAFISA TARAFA--RC SENYAMULE

Imetumwa : March 12th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amempongeza Mhe. Rais kwa kuendelea kuimarisha mazingira bora kwa Watumishi wa Umma sanjari na huduma nzuri kwa Watanzania. Hayo yamebainishwa katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya Machi 12, 2025 kwenye Ofisi ya Afisa Kata ya Rudi katika Halmashauri ya Mpwapwa.


"Nimshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kuimarisha mazingira mazuri kwa Watumishi wa Umma lakini pia kwa Watanzania kupata huduma. Afisa Tarafa ni kiungo muhimu sana kati ya Serikali kuu na Serikali za mitaa, ndio maana dhamira ya Mhe. Rais kuunganisha huduma hizi ni ili ziweze kufanya vizuri kwa Mkoa wetu” Mhe. Senyamule.


Akisoma taarifa ya Mradi huo, Mhandisi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bw. Frank Mabubu, amesema mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi 150,000,000 ukiwa na lengo la kuboresha mazingira ya kutolea huduma kwa Afisa Tarafa na kurahisisha utoaji huduma kwa Wananchi.


Mradi mwingine uliotembelewa na Mkuu wa Mkoa huyo ni Ofisi ya Afisa Tarafa Kata ya Mpwayungu, Halmashauri ya Chamwino, mradi ambao umegharimu kiasi cha shilingi 150,000,000 na upo katika hatua za umaliziaji.


Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika eneo hilo baada ya kukagua Mradi, Mhe. Senyamule ametaja malengo mawili makubwa ya ujenzi wa Mradi huo.


“Lengo la majengo haya ya Serikali ni ubora wake ili kutoa mfano kwa wananchi juu ya ujenzi wa nyumba bora lakini pia ni wananchi kupata huduma nzuri katika eneo hili kwa kutatua changamoto zao. Tunategemea atakayetumia ofisi hii awe na jambo moja tu la kutatua changamoto za wananchi”. Amesema Mhe. Senyamule.


Ziara ya Mkuu wa Mkoa ilihitimishwa kwa kutembelea Mradi wa ujenzi wa nyumba za kupumzikia viongozi wa Serikali katika eneo la Njedengwa Jijini Dodoma ambao unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 2.9 na utekelezaji wake umefikia 95% kwa nyumba kuu, uzio 98% na vibanda vya ulinzi vipo hatua za umaliziaji.




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.