• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SHILINGI BILIONI 38.6 ZIMENUNUA DAWA NA VIFAA TIBA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE DODOMA

Imetumwa : October 6th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Imebainishwa kuwa katika fedha za miradi ya maendeleo zilizopokelewa katika Mkoa wa Dodoma katika kipindi cha miaka minne, shilingi Bilioni 38.6 zimetumika kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba ambavyo vimewezesha watoa huduma za Afya kwa ngazi zote kuweza kuhudumia wananchi na kuokoa maisha kwa kiwango kikubwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amebainisha hayo wakati akizungumza na Madaktari Bingwa pamoja na Wauguzi wabobevu maarufu kama ‘Madaktari wa Samia’ ambao wamewasili kwa ajili ya awamu ya nne ya utoaji huduma za Kibingwa Mkoani hapa na kupokelewa katika ukumbi wa Ofisi yake Jijini Dodoma leo Oktoba 06, 2025

“Katika fedha zilizoletwa Mkoa wa Dodoma, tumetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 38.6 kununua dawa na vifaa tiba ambapo uwekezaji huu umeongeza idadi ya vituo vya Afya. Kazi mnayokwenda kuifanya ni kuwawezesha wahudumu wa afya kutoa huduma za dharura hivyo, mnachokwenda kukifanya ni kuokoa maisha ya watu”.

Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Khatibu Kazungu, amesema huduma za Madaktari Bingwa ni jambo ambalo nchi imejiwekea katika Dira 2050 na utekelezaji wake unalenga kuimarisha Afya za wananchi ili waweze kufanya uzalishaji katika Taifa kwani Serikali imetumia rasilimali nyingi kuwajenga Wataalam hao.

Nae Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Bi. Subira Abdallah, amesema lengo la mpango wa Serikali kupeleka Madaktari Bingwa na Wauguzi wabobevu kwenye Hospitali za Halmashauri ni kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi lakini pia kuwajengea uwezo Wataalamu katika ngazi ya msingi waweze kuendeleza ujuzi watakaoupata.

Vile vile, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Thomas Rutachunzibwa amesema, kwa awamu tatu walizopita Madaktari hao katika Mkoa huu, waliweza kuwafikia takribani wananchi 7,200 na awamu ya nne iliyoanza Septemba 15 hadi Novemba 14, 2025 Madaktari 42 wa kada tofauti wamewasili kwa ajili ya kutoa huduma huku wakitarajia kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Madaktari wa Samia wanatarajia kutoa huduma kwenye Mkoa wa Dodoma katika Hospitali za Halmashauri 7 (Bahi, Chemba, Chamwino, Kondoa TC, Kondoa DC, Kongwa na Mpwapwa) kuanzia Oktoba 06 hadi 10, 2025 hivyo wananchi wenye uhitaji wa huduma za kibingwa wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo adhimu.

#DodomaFahariyaWatanzania

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigakura

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI INA DHAMIRA YA KILA MWANAMKE KUJIKOMBOA KIUCHUMI

    October 09, 2025
  • SACCOS NI FURSA KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA WANAWAKE

    October 11, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DODOMA

    October 09, 2025
  • KIWANDA CHA MVINYO KUFUFUA MATUMAINI YA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA

    October 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.