• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SKAUTI MKOA WA DODOMA WAASWA KUANZISHA PROGRAMU ZA KUVUTIA VIJANA KUJIUNGA

Imetumwa : October 4th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wito umetolewa kwa Chama cha Skauti Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanachama wake wanabuni programu za kuvutia vijana wengi kujiunga na Chama hicho ili kuimarisha vizazi vijavyo vyenye maadili, kujitegemea, kujitolea na kushiriki shughuli mbalimbali za jamii.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Decca Medics Limited Dr. Gustavus Deusdedit, ameyasema hayo alipokua Mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Mkoa wa Dodoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Jengo la Mkapa Jijini hapa.

“Skauti hufundisha vijana ujasiri na Moyo wa kujitolea kushiriki shughuli mbalimbali za jamii ili kukuza Viongozi wa kesho wenye maono na waadilifu hivyo, nitoe wito kwenu kuhakikisha mnabuni programu za kuvutia vijana wengi kujiunga na Skauti ili kuimarisha vizazi vijavyo kwani ni wajibu wenu kuwalea vijana wa kesho kuwa wenye maadili mema.”

Aidha, Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dodoma ALT Salama Katunda, amesema Mkutano huo ngazi ya Mkoa ndio chombo cha juu cha kiutawala na maamuzi kuhusiana na yote yanayokwenda kutendeka katika ngazi ya Mkoa na unahusisha wajumbe  watakaoridhia taarifa ya utendaji pamoja na kuazimia Mikakati ya Skauti kwa mwaka 2026.

Akisoma risala ya Chama hicho, Bw. Paul Makubi amesema Chama kimeimarisha uhusiano na wadau mbalimbali ambao wanashirikiana katika malezi ya vijana kwa kufanya semina za kujengeana uwezo ambapo baadhi ya wadau hao ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi za Halmashauri, Polisi Zimamoto, 'Red cross na  Taasisi za Kidini.

Chama cha Skauti ni Taasisi ya malezi ya Vijana inayotambulika ulimwenguni ambapo ilianzishwa mwaka 1905 na iliingia Tanzania mwaka 1907 ikiwa na lengo la kuwalea Vijana kimwili, kiroho na kiakili ili wawe shupavu, wakakamavu na wenye manufaa kwenye jamii kwa kuimarisha nidhamu miongoni mwao.


#DodomaFahariyaWatanzania

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigakura

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI INA DHAMIRA YA KILA MWANAMKE KUJIKOMBOA KIUCHUMI

    October 09, 2025
  • SACCOS NI FURSA KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA WANAWAKE

    October 11, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DODOMA

    October 09, 2025
  • KIWANDA CHA MVINYO KUFUFUA MATUMAINI YA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA

    October 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.