• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

STAMICO WAKABIDHI MAKONTENA MAWILI YA MKAA SAFI KWA KIKUNDI CHA WANAWAKE NA SAMIA

Imetumwa : June 24th, 2025

Na. Hellen M. Minja

      Habari - DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma unaendelea na jitihada za kutunza mazingira kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwa ni katika kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,  ambapo kwa ufadhili wa Shirika la Madini Nchini (STAMICO), kikundi cha Wanawake na Samia Mkoani hapa kimepokea Makontena mawili yatakayotumika kama Maduka au stoo kwa ajili ya Mkaa safi wa kupikia.

Hafla ya kuzindua na kupokea Makontena hayo ambayo ndani yake yalikua na magunia ya Mkaa safi uliopewa jina la 'Rafiki Briquettes', imefanyika, mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule mnamo Juni 23, 2025 katika eneo la Sabasaba ambapo Kontena moja litapatikana hapo na jingine litapatikana  Nzuguni Jijini hapa.

"Umeponya macho na vifua vya hawa Wanawake ambao sasa wanatumia nishati safi kupikia, lakini pia tungekua na nafasi ya kwenda porini, ungeona ni kwa kiasi gani umeokoa mazingira ya Nchi Yetu ambayo yanatusaidia kupata hewa safi, mvua na faida nyingine lukuki zinazoletwa na utunzaji wa mazingira". Amesema Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse, amesema Shirika lake lina dhamira ya dhati kuichukua ajenda ya Mhe. Rais Samia na kuipeleka mbele mpaka kufikia malengo aliyojiwekea ya kwamba ifikapo mwaka 2034, asilimia 84 ya Watanzania wawe wamehama kutoka kwenye matumizi ya nishati chafu na kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza kwa niaba ya kikundi hicho, Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma Bi. Fatma Madidi, amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuona uhitaji wa kundi hilo kuwezeshwa kupitia biashara ya nishati safi ya Mkaa wa kupikia kwani ameinua maisha ya Wanawake hao kiuchumi kwa kiasi kikubwa.

Kikundi cha Wanawake na Samia kilipewa uwakala wa uuzaji na usambazaji wa Mkaa huo na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka 2023 ,ambapo Shirika la STAMICO liliahidi kuwaletea Kontena sambamba na Mkaa huo unaotengenezwa kwa kutumia Makaa ya mawe, hatimaye ahadi hiyo imetimia. Makontena hayo yapo 26, yanatarajiwa kusambazwa kwa vikundi hivyo nchi nzima.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#wekezadodomastawishadodoma

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • VODACOM TANZANIA KUPANDISHA HADHI MINARA YAO KUIMARISHA MAWASILIANO DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.