• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TBL YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI, KUJENGA MKOANI DODOMA KIWANDA CHA BIA KIKUBWA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Imetumwa : November 21st, 2018

Kampuni ya kutengeneza, kuuza na kusambaza bia hapa nchini “Tanzania Breweries Limited - TBL” imeunga mkono azma ya Tanzania ya Viwanda na jitihada za Rais Magufuli za kuhamishia Serikali Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Nchi kwa kuamua kujenga kiwanda kikubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati cha Kutengeneza Bia Mkoani Dodoma, ujumbe wa TBL umethibitisha ukiwa Mkoani Dodoma katikati ya wiki hii.

Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TBL Bi. Georgia Mutagahywa amesema kuwa kiwanda hiki kitakuwa kikubwa zaidi hapa nchini na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha karibu mara mbili ya kiasi cha bia kinachozalishwa sasahivi na viwanda vyote vinne vya TBL vilivyopo Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.

Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TBL Bi. Georgia Mutagahywa (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao na uongozi wa Mkoa wa Dodoma

Nae Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Mhandisi Waziri Jemedari amesema kuwa ujenzi wa kiwanda hiko utafanyika ndani ya miezi 18 kuanzia mwaka 2019 na kukamilika mwaka 2020 na kugharimu takribani Dola za Marekani Milioni 400. Kufuatia uwekezaji huo TBL wanahitaji eneo la Ardhi lenye ukubwa wa Ekari takribani 250 Mkoani Dodoma ambazo mbali na Kiwanda cha Bia, watatengeneza pia kiwanda cha kusindika Mvinyo na kiwanda cha pombe kali (Konyagi) ambapo mipango ya mbeleni ni kukihamishia jijini Dodoma kiwanda cha Konyagi kilichopo Dar es salaam. Mhandisi Waziri amesema kuwa Makao Makuu ya TBL Tanzania nayo yatahamishiwa hapa Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Nchi.

Kwa mujibu wa Mhandisi Waziri kiwanda hiko kitatoa ajira zaidi ya 450 ambazo zitakuwa chini ya TBL na ajira zingine zaidi ya 1500 ambazo zitakuwa zinafanywa na makampuni na wajasiriamali wengine hapa Mkoani Dodoma. Amesema kuwa kiwanda hiko mbali na kulipa kodi mbalimbali kitakuza sekta ya Kilimo cha zao la Mtama na Zabibu ambayo yanastawi vizuri kwenye Mkoa wa Dodoma kwa kuzalisha soko kubwa la mazao hayo yanayotumika kutengenezea bia, mvinyo na pombe kali.

Kikao cha pamoja kati ya wawakilishi wa TBL na Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kikiendelea chini ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Mahenge

Kufuatia uwekezaji huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameipongeza kampuni ya TBL na kusema kuwa uwekezaji huo una manufaa kwa Taifa na kwamba unaunga mkono azma ya Mhe. Rais Magufuli ya Tanzania ya viwanda na azma ya kuhamishia Serikali hapa Dodoma Makao Makuu. Dkt. Mahenge amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndg. Godwin Kunambi kuhakikisha eneo la Ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hiko linapatikana mara moja ili mipango ya ujenzi iendelee.

Dkt. Mahenge amesema kuwa Serikali itafanya kila linalowezekana ili TBL wafanikiwe kuwekeza kiwanda hiko na kuongeza kuwa utawekwa mpango wa pamoja unaoonesha ratiba zote muhimu za majukumu katika mradi huo mkubwa na kuwa mpango huo utaonesha jukumu la kila mdau kwa maana ya majukumu ya serikali na majukumu ya TBL.

Nae Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndg. Godwin kunambi amewahakikishia TBL kuwa eneo lenye kutosheleza uwekezaji huo litapatikana kwa mujibu wa mpango kabambe wa uendelezaji wa mji na kuwa eneo hilo litakuwa na miundombinu wezeshi kwa shughuli za viwanda, kwa mujibu wa Bw. Kunambi kazi ya kutembelea maeneo yanayofaa kwa uwekezaji huo inaanza wiki hii.

Afisa Uwekezaji wa Jiji la Dodoma Ndg. Abeid Msangi akiwapitisha kwenye Ramani ya Maeneo ya Viwanda Maafisa wa TBL 

(PICHA NA HABARI NA OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA)

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.