• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TBS YATOA VYETI VYA UBORA KANDA YA KATI

Imetumwa : April 28th, 2023


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu amewatunuku Vyeti na Leseni wafanyabiashara na wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa Ubora wake na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wazalishaji wa kanda ya kati (Dodoma, singida na Tabora) pamoja na Iringa na kuwaasa wazalishaji kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa viwandani zinazingatia kanuni bora za uzalishaji.

Hafla hiyo imefanyika leo tarehe Aprili 28,2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

"Kazi hii iliyofanywa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, kupitia TBS ni mwendelezo wa azma ya Serikali katika kuhakikisha wazalishaji wa bidhaa viwandani kama wadau muhimu wa maendeleo ya ubora na usalama wa bidhaa, wanazalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya Viwango vya ubora Kitaifa na kimataifa na kuhakikisha Watanzania wananunua na kutumia bidhaa zenye ubora na ambazo ni salama kwa afya zao na mazingira

"Nitoe rai kwenu nyote ambao mmeshiriki kutimiza wajibu wenu kwa kuweka uzalendo mbele kwa kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na kusambazwa nchini ni bora na salama. Sambamba na hilo niwaagize muendelee kuwa mabalozi wazuri kwa wazalishaji wengine ambao bado hawajathibitisha ubora wa bidhaa zao, lengo likiwa ni kuwa na soko lenye bidhaa bora kwa matumizi ya ndani na nje ya Tanzania, ninaamini kuwa hafla hii ni njia mojawapo ya kuleta tija katika udhibiti wa bidhaa ndani ya Mkoa wetu, Kanda na Taifa kwa ujumla "amefafanua Gugu

Naye, Meneja wa Kanda ya Kati Bw. Nikonia Mwabuka ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania amesema wazalishaji kuendelea kuwa waaminifu na kuzingatia maelekezo wanayopatiwa na Shirika la Viwango ili bidhaa ikithibitishwa ubora ni kuhakikisha kuwa afya za wananchi na mazingira zinalindwa kwa kila mmoja .

"Bidhaa ikithibitishwa ubora wake na nchi wanachama ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki bidhaa hiyo itaingia katika nchi wanachama pasipo kukaguliwa na kupimwa tena ili kutambua ubora wake ." Amesema Mabuka

Jumla ya Vyeti na Leseni 29 za wafanyabiashara na wazalishaji zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wazalishaji wa kanda ya kati (Dodoma, singida na Tabora) pamoja na Iringa.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.