• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TIMU YA UMITASHUMTA 2025 MKOA WA DODOMA YASISITIZWA NIDHAMU,UPENDO NA KUJITUMA

Imetumwa : May 30th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wawakilishi wa timu ya Mkoa wa Dodoma kwenye Umoja wa Michezo kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2025 inayotarajiwa kufanyika Mkoani Iringa, wametakiwa kuliheshimisha jina la Mkoa kwa kuwa na nidhamu, kupendana na kujituma ili kuhakikisha makombe yote yanarudi Dodoma.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mkoa wa Dodoma ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Mwalimu Justin Machela, ameyasema hayo Mei 30, 2025 wakati wa hafla fupi ya kutangaza timu ya Mkoa itakayowakilisha kwenye mashindano hayo Kitaifa Mkoani Iringa iliyofanyika katika  Shule ya Sekondari Dodoma.

“Makombe yanapatikana kwa namna tatu, kujituma sana uwanjani, nidhamu na kupendana ninyi kwa ninyi. Mkuu wa Mkoa anatamani kila tunaposhindana Dodoma tuwe wa kwanza kwa vigezo na viwango vya hali ya juu. Waalimu ambao tunakwenda na watoto, kazi yetu ni kuwasimamia na kuendelea kuwafundisha, kuhakikisha nidhamu ya watoto inakua juu na ya yetu pia inakua juu”.

Kadhalika, Umoja wa Walimu Wakuu Tanzania (TAPSHA) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mwalimu James E. Manary, wameunga mkono juhudi za kuwawezesha watoto hao kukaa kambini kwa kipindi ambacho wanasubiri safari ya kuelekea Iringa kwa kutoa vyakula na fedha taslimu.

“Sisi vijana wa TAPSHA, tunakabidhi vitu vyenye thamnai ya shilingi 3,380,000 ambavyo ni vyakula, jezi za ‘football’ 22, jezi za ‘netball’ 10 lakini pia ‘tracksuit’ ambazo tumezitoa kama motisha kwa mtoto atakayefanya vizuri pia tunatoa fedha taslimu shilingi 730,000 ambazo 600,000 kwa ajili ya nyama na 130,000 ya vitafunwa”.

Katika hatua nyingine,Afisa elimu awali na msingi Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mwl. Josephat Ambilikile, amezungumzia siri ya mafanikio ya Chemba kwani wamebeba vikombe vingi sambamba na kuibuka washindi wa jumla kwenye mashindano hayo ngazi ya Mkoa ambapo amesema ni ushirikiano mkubwa ulipo katika idara ya elimu Msingi na jitihada za Walimu shuleni.

Mashindano ya kutafuta timu ya Mkoa kwa ajili ya kushiriki UMITASHUMTA 2025, yameshirikisha  wanafunzi  960 kutoka shule za msingi za Halmashauri zote 8 za Mkoa wa Dodoma ambapo mchujo ulifanyika na kupatikana wanafunzi 120 kwenye timu hiyo ya michezo mbalimbali ambao watakaa kambini hapo kwa siku 6 kabla ya kuelekea Mkoani Iringa.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.