• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TUMERIDHISHWA NA UTEKELEZAJI NAUBORA WA MIRADI YA CHEMBA-JAWADU

Imetumwa : November 14th, 2023

Kamati ya siasa ya Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Katibu Wa Itikadi na uenezi (NEC ) Mkoa wa Dodoma Bw.Jawadu Mohamed imewapongeza wasimamizi wa miradi inayotekelezwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ikiwemo Miradi ya Shule na Hospitali kwa kuzingatia ubora na ufanisi unaotakiwa.

Akizungumza na baadhi ya viongozi walioshiriki katika ziara ya ukaguzi wa Miradi hiyo Bw. Mohammed amewataka watumishi wa Umma kuitangaza na kuwa Mabalozi Wazuri wa Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema "ni lazima tuwe na watu makini wa kufuatilia miradi inayoletwa na Rais wetu ili wananchi wasiwe na changamoto katika kupata huduma na ndio maana zimejengwa shule na Hospitali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na zinazostahili.

“Serikali ipo imara na imedhamiria kuhakikisha wananchi wanapata huduma za umeme, maji, mabweni, madarasa na majengo yote yanakua kwenye ubora na uimara wa Hali ya juu.Ni lazima miundombinu zote zikamilike kwa wakati kama mikataba inavyotaka hatufikirii kuona miradi inavuka muda wake wa utekelezaji,” Amesema Bw. Mohamed.

Pia Bw. Mohamed amesisitiza suala la upandaji Miti kwa Kila mradi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa bora na imara hivyo kudumisha Sera ya Serikali ya Mkoa ya "Kijanisha Dodoma".

Kamati hiyo ilipata fursa ya kutembelea mradi wa Barabara kwa kiwango cha lami uliogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 599, ujenzi wa kituo cha afya Farkwa uliopokea kiasi cha Shilingi Milioni 500, Ujenzi wa Shule ya Msingi na awali Sankwaleto uliopokea kiasi cha shilingi Milioni 396, ujenzi wa Zahanati ya Sankwaleto ambao umepokea kiasi cha Shilingi Milioni 97, na ujenzi wa Mradi wa maji Babayu uliopokea kiasi cha shilingi Milioni434.

Ukaguzi wa Miradi mbalimbali unaofanywa na Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wa Kamati Bw. Mohmed ni muendelezo wa ziara ya kikazi wanayoifanya katika halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Dodoma. ‎

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.