• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UONGOZI WA MKOA WA DODOMA NA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO WAKUBALIANA KUBORESHA UWANJA WA NANE NANE NZUGUNI NA KUWEZESHA SHUGHULI ZA KILIMO KWA WAKULIMA MKOANI DODOMA

Imetumwa : August 30th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na kukubaliana juu ya mambo makubwa mawili; kuboresha uwanja wa maonesho ya kilimo na mifugo Nane Nane Kanda ya kati uliopo Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kuwezesha mitaji kwa Vikundi vya wakulima na wajasiriamli wanaoendesha shughuli za Kilimo na uchakataji ama uongezaji thamani ya mazao ya kilimo hapa Mkoani Dodoma.

Ujumbe huo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara Ndugu Augustino Chacha aliyeambatana na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Benki hiyo Ndugu Geofrey Mtawa ambao kwa pamoja na Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Rugimbana walikubaliana kuubadili Uwanja wa Nane Nane Nzuguni kuufanya kuwa na hadhi ya kimataifa na kuvutia wawekezaji mbalimbali kutoka hapa nchini na nje ya nchi kuwekeza uwanjani hapo na kushiriki kwenye Maonesho ya Nane Nane.

Mheshimiwa Rugimbana alibainisha kuwa uwanja wa Nane Nane wenye ukubwa wa Ekari zisizopungua 400 utagawanywa katika maeneo makubwa mawili ili kuruhusu eneo moja kuanzisha ukanda maalumu wa Viwanda vinavyohusiana na Utengenezaji na uchakataji wa Bidhaa zinazotokana na kilimo na mifugo lakini pia upande wa pili utaendelezwa kisasa kwa ajili ya kuendesha shughuli za Maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi, pia utawekewa huduma na miundombinu yote muhimu itakayouwezesha Uwanja huo kuweza kutumika kipindi cha mwaka mzima kwa shughuli za kilimo, mifugo, biashara, huduma za jamii, Burudani na michezo mbalimbali na hivyo kuwa na manufaa zaidi kuliko ilivyosasa.

kwa mujibu wa mazungumzo ya pande hizo mbili Ukanda maalum wa kuanzisha viwanda katika Uwanja huo wa Nane Nane Nzuguni utapangiliwa vizuri kitaalamu na kuwekewa miundombinu yote muhimu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania watakaribishwa kuja kuanzisha viwanda mbalimbali kama sehemu ya kuitikia maelekezo ya serikali ya kuanzisha viwanda na kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya uchumi wa kati.

Viwanda hivyo vinatarajiwa kutumika kuchakata mazao ya kilimo na mifugo na kuyaongezea thamani lakini pia teknolojia mbalimbali za kuboresha na kuongeza tija za shughuli za kilimo na mifugo. Mkuu wa Mkoa Rugimbana ameahidi kuwaunganisha Benki ya TADB na wadau wengine wa maendeleo waliojitokeza kwenye Mkoa wa Dodoma kuendeleza shughuli za kilimo na mifugo, lakini pia kuhusisha viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma na Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Dodoma na Wataalamu wa Kilimo ili kuwa na programu ya pamoja itakayotoa matokeo makubwa zaidi na tayari ameshaunda kikosi kazi kwa lengo la kushughulikia mipango hiyo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB Ndugu Augustino Chacha amebainisha kuwa wao kama Benki wanawezesha shughuli zote zilizopo kwenye mchakato wa kilimo na uzalishaji mazao ya kilimo, wanawezesha wakulima na wajasiriamali (wachakataji na wasindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo) wadogo, wakati na wakubwa na hata baazi ya taasisi kama zile zinazoshughulika na utafiti na uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali ya kilimo kwa lengo la kumaliza changamoto ya ukosefu wa mbegu bora unaowakabili wakulima na kurudisha nyuma tija ya shuguli zao za kilimo.

Pia amebainisha kuwa wao kama Benki wanaweza kushirikiana na wadau wa Maendeleo wanaounga mkono sekta ya kilimo kwenye Mkoa wa Dodoma na kuwa wako tayari kuunganisha nguvu zao pamoja na wadau hao kuhakikisha programu ya uendelezaji kilimo Mkoani Dodoma inaleta mafanikio makubwa.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.