• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Upandaji Miti Shule ya Msingi na Sekondari Mvumi Makulu

Imetumwa : June 5th, 2022


Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma inaendelea na zoezi la upandaji Miti katika maeneo tofauti tofauti kuelekea kilele cha siku ya Mazingira Duniani June 05 ambapo siku ya tarehe 04 June, zoezi hilo lilifanyika katika shule ya msingi na sekondari Mvumi Makulu inayopatikana katika Wilaya ya Chamwino.Katika zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi Gift Msuya kama Mgeni rasmi na takribani Miti 3,000 ilipandwa katika eneo hilo.

Wadau tofauti tofauti wanaoshughulikia utunzaji wa Mazingira nchini kama Wakala wa Misitu Tanzania TFS, Lead Foundation (Kisiki hai), na Chuo Kikuu cha Dodoma, UDOM na wengine wengi, walijitokeza kushiriki katika zoezi hilo na walipata nafasi ya kutoa neno ambapo TFS wamesema kuwa wana jukumu la kutunza na kuendeleza rasilimali Misitu nchini na zoezi hilo ni muendelezo wa kampeni ya kuikijanisha Dodoma iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan mwaka 2018 alipokua Makamu wa Rais.Tangu hapo, TFS iliendelea na zoezi la upandaji Miti ambapo Dodoma Jiji ndio alikua mdau Mkubwa kwa kufanikisha upandaji wa Miti zaidi ya Milioni Tano mpaka Sasa na kwa Mwaka huu pekee tayari wamepanda Miti 780,000.

Baadhi ya wadau wa Mazingira walioshiriki katika zoezi hilo wamehamasisha wananchi kutunza Mazingira kwa njia za asili ili kuendeleza mpango mkakati wa kuifanya Dodoma ya kijani kuepuka hali ya ujangwa iliyokua ikiinyemelea. Pia Wadau wa Lead Foundation maarufu kama "Kisiki hai",  wamefanikiwa kutoa elimu ya utunzaji wa Mazingira na kuanzia mwaka 2018 mpaka Sasa, viongozi 365 wa vijiji vinavyopatikana katika Wilaya za Dodoma na wakulima 175,000 wameelimishwa.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, UDOM, Prof. Donald Mpanduji naye alipata nafasi ya kuongea machache na alisema kuwa Chuo chake ni Wadau wakubwa wa utunzaji wa Mazingira kwani kinatoa taaluma ya Misitu na wameshapanda takribani Miti 20,000 katika maeneo tofauti tofauti huku kwa Mwaka huu pekee wakiwa wameshapanda Miti 3,000."Jukumu kubwa la Chuo Kikuu cha Dodoma ni kutoa elimu na ushauri wa kimaendeleo kwa jamii zinazokizunguka Chuo juu ya utunzaji wa Mazingira" Prof. Mpanduji.

Bi Khadija Yusuph, Balozi wa Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, alipata fursa ya kuongelea kampeni ya "SOMA NA MTI" yenye lengo la kuwaelimisha wanafunzi umuhimu wa kupanda Miti na amesema kila mmoja ana haki ya kutunza Mazingira hivyo wanafunzi wanatakiwa kujifunza hilo tangu shuleni kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anapoanza shule anapanda mti wake na kuutunza mpaka siku atakapohitimu masomo yake katika shule husika.


Akihitimisha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Bi Msuya alitoa maelekezo ya Mhe. Mtaka kwa Wadau wanaoshughulikia utunzaji wa Mazingira kwa kuwataka TFS kuzalisha Miche ya kutosha ya Matunda kwani Matunda yatasaidia kuboresha afya za wanajamii pia amewataka viongozi na wadau wa Mazingira kutoa Elimu ya utunzaji wa Mazingira kwa wananchi na kuhakikisha pia wanakomesha matumizi ya mifumo ya plastiki ambayo ilipigwa marufuku hapo awali lakini inaonekana kuendelea kutumika kwa wingi katika baadhi ya maeneo.Bi. Msuya aliongeza kuwa upandaji Miti katika eneo la Mvumi Makulu umefanyika kwa kuwa eneo hilo lina historia kubwa kwa viongozi wetu enzi za kupigania Uhuru wa nchi hivyo linapaswa kuenziwa. Aidha, amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kupanda Miti katika maeneo yao kwani TFS wanazalisha Miche mingi na wanaigawa bure kwa yeyote atakayehitaji kupanda katika eneo lake.


MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.