• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KILIMO DODOMA UNARIDHISHA

Imetumwa : November 11th, 2023

Kamati ya Kudumu ya Bunge la Bajeti imeridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo mradi wa Bwawa la Membe na mradi wa Skimu ya umwagiliaji Chinangali chini ya Mradi wa Building Better Tomorrow (BBT) katika Wilaya ya Chamwino.

Akizungumza Leo Novemba 11,2023 Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mbunge wa Kilindi Mkoani Tanga Mhe. Omary Kigua wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyoanzia Mkoa wa Dodoma na inatarajia kufanyika kwa siku saba katika Mikoa mingine tofauti tofauti ikiwemo Manyara, Arusha, Singida, Tabora ,Iringa na kukamilika katika Mkoa wa Mbeya.

Amesema ziara hiyo ina lengo la kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Wizara ya Kilimo.

“Tumeridhika na shughuli zinazoendelea hapa na kiasi cha fedha ambacho kimetumika hakika kinasadifu kwamba kazi mnaisimamia vizuri ". Ameeleza Mhe. Kigua

Aidha, amewahimiza  wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali popote utakapo hitajika kwani kukamilka kwa mradi huo itakuwa chachu kwa wananchi wote ambao wapo jirani na maeneo hayo ya miradi kwa  kuwa wao ndio wanufaikaji  wa kwanza na ndiyo dhamira ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni kuinua maisha ya wananchi wa chini.

Kwa Upande Wake, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ametumia fursa hiyo kuelezea azma ya Serikali katika kuhakikisha wanamuwezesha mkulima kuzalisha kipindi chote cha mwaka  bila kutegemea mvua.

“ Lengo letu kama Wizara tunataka Wananchi waweze kufanya shughuli za Kilimo mara mbili hadi tatu kwa mwaka wasitegemee mvua , Pia  mradi huu  hautakua kwa ajili ya kilimo tu bali hata wafugaji  watatengenezewa banio kwa ajili ya kunyweshea ng'ombe na shughuli za uvuvi pia zitafanyika.” Amesema Silinde

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amemshukuru Mhe. Rais kwa kufanya Mapinduzi ya Kilimo ndani ya Mkoa huo ambayo yatasaidia kuondoa njaa ,udumavu na kitakuwa chanzo cha uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Ameahidi kuendelea kuwa karibu na wakandarasi ili fedha zilizotolewa na Serikali ziweze kufanyiwa kazi husika na kwa ufanisi .

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.