• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UWANJA WA MPIRA WA MIGUU WA KIMATAIFA RASMI KUJENGWA NZUGUNI , DODOMA

Imetumwa : February 13th, 2025

Na: Hellen M. Minja,

Habari - DODOMA RS


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Palamagamba Kabudi, leo Februari 13, 2025, ameshuhudia utiaji saini Mkataba wa kuanza rasmi Ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu utakaokuwa na uwezo wa kuketisha watazamaji 32,000 kwa mara  moja katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma.


Akizungumza na hadhara iliyojitokeza kushuhudia tukio hilo, Waziri Prof. Kabudi ametoa wito kwa Mamlaka zinazohusika na vibali vya Ujenzi, kuharakisha upatikanaji wa vibali hivyo ili zoezi lianze mara moja na kukamilika kwa wakati uliopangwa.


"Ili kukamilisha azma hii kwa wakati, baadhi ya masuala ya muhimu kama kupatikana kwa vibali vya Ujenzi kutoka Ardhi, zimamoto, mazingira, huduma za umeme, maji na Barabara za Mawasiliano zinatakiwa kufika kwenye eneo la Mradi ili kufikia lengo la kuwapa wananchi uwanja wenye hadhi ya Makao Makuu ya nchi". Prof. Kabudi


Aidha, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Khamis Mwinjuma (MB) amesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Mhe. Dkt. Samia, wameweza kufanya mambo mengi kwenye Ujenzi wa miundombinu ya michezo ikiwemo ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa, uwanja wa Uhuru, uwanja wa kisasa wa michezo Arusha na mingine mingi.


Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa amesema uwanja huo utagharimu fedha kiasi cha shilingi Milioni 310 ambayo itagharamiwa na Serikali kwa 100% huku ujenzi wake ukitekelezwa na Kampuni ya Ujenzi kutoka nchini Italia ya Limonta.


Kadhalika, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amebainisha kuwa; "Moja ya vipaumbele vya Mkoa ni utalii wa michezo ikiwemo mpira wa miguu hivyo, tulikua tunaandika uwanja ambao hatujauona kwa macho lakini tukawa tunaishi kwa imani kuwa uwanja huu utatokea na utaleta watu wengi hivyo, tujipange kwa utalii huu wa michezo uwe na tija kwa wananchi wa Dodoma"


Nae, Mbunge wa Jimbo la Dodoma na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, amempongeza Mhe. Rais kwani wananchi wake walikua na shauku kubwa ya kuona uwanja huo unajengwa hapa Dodoma na leo wameshuhudia tukio kubwa la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa kuanza rasmi Ujenzi wa uwanja huo.




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#birthdayyangumtiwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.