• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

“VICOBA TUMIENI FURSA KWA KUFANYA BIASHARA NA SERIKALI “- RC SENYAMULE

Imetumwa : October 3rd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Vikundi vya huduma ndogo za kifedha vinavyopatikana katika Jiji la Dodoma (VICOBA), vimetakiwa kutumia fursa kufanya biashara na Serikali kupitia miradi mikubwa ya uwekezaji inayofanyika kwenye Makao Makuu ya nchi kwani thamani yao kwa Serikali ni kubwa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akifunga kikao alichokiitisha kuzungumza na viongozi wa vikundi hivyo kwenye ukumbi wa Safina Jijini Dodoma Oktoba 03, 2025 juu ya kukua kiuchumi kwa kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana hapa.

“VIKOBA mna thamani kubwa kwenye Serikali hii kwa sababu zipo fursa nyingi za kufanya biashara na Serikali lakini fursa hizi tutazipata tukichukua hatua. Nitoe Wito kwa Dodoma, tutumie fursa hizo kwani ofisi zetu zipo wazi kwa ajili yenu, wote mna haki ya kupata huduma kwenye ofisi za Serikali.”

Aidha, Mratibu Msaidizi wa Huduma ndogo za kifedha Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bi. Farida Mayega amesema Jiji linatekeleza usajili wa huduma ndogo za kifedha kwa mujibu wa Sheria iliyopitishwa mwaka 2018 ambayo inalenga kulinda watumiaji wa huduma hiyo pindi wanaposajili vikundi vyao na kutambulika rasmi.

Akitoa mada kuhusu Mikopo kwa wanavikundi hao wa VIKOBA, Afisa kutoka Benki kuu yaTanzania Bw. Fanuel Kijoji, amewaasa wanavikundi kuweka akiba ya fedha ili kuepuka mikopo isiyo ya lazima ambayo wakati mwingine haipelekwi kwenye uzalishaji hali inayowaumiza kiuchumi.

Jiji la Dodoma lina vikundi vya VICOBA 351 vilivyosajiliwa vikiwa na wanaume 568 na wanawake 4,010, takribani vikundi 191 vimesajiliwa kwenye robo ya mwaka huu na usajili wake huanzia ngazi ya Kata kupitia Afisa Ustawi wa Jamii huku wanakikundi wakinufaika kushiriki kwenye fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia Taasisi zake.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#nimejiandikishanitapigakura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • “TUSIMAME IMARA JUU YA KULINDA AMANI YA NCHI YETU - RC SENYAMULE

    October 07, 2025
  • DKT. KAZUNGU ATOA WITO KWA WADAU WA TAKWIMU KUZINGATIA USAHIHI

    October 07, 2025
  • JIJI LA DODOMA KUNUFAIKA NA TEKNOLOJIA KUTOKA JAMHURI YA CZECH

    October 07, 2025
  • “VICOBA TUMIENI FURSA KWA KUFANYA BIASHARA NA SERIKALI “- RC SENYAMULE

    October 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.