• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIJANA WANAOPATIWA MKOPO YA KILIMO KUFUATILIWA KWA MFUMO MAALUM

Imetumwa : August 4th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Agizo limetolewa la kuundwa kwa Mfumo maalum wa kufuatilia fedha zinazotolewa na Taasisi za Kifedha za Serikali kwa Vijana wanaojishughulisha na kilimo kwani fedha hizo zinatolewa kwa malengo mahususi na sio sadaka.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya mazao Dkt. Stephen J. Nindi, ametoa agizo hilo alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa dirisha la mikopo kwa vijana wanaojihusisha na kilimo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Viwanja vya maonesho ya Nanenane 2025 Nzuguni Jijini Dodoma.

“Utengenezwe mfumo imara wa kufuatilia hii fedha kwani sio ya bure, kuna watu sehemu fulani wameteseka, Serikali imekusanya inakupatia wewe, ‘it’s not fo free’. Kwa hiyo lazima twende tuwafundishe mfano wa SACCOS zilizofanya viizuri kwani haiihitaji elimu kubwa kumfuatilia mtu, tusiwape hii fedha kama sadaka”.

Kadhalika, Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Pembejeo – AGITF Bw. Itandula Gambalagi amesema watafanya ufuatiliaji wa fedha inayotoka kwa dhamana hiyo ili kuhakikisha zinarejeshwa na kuwafikia walengwa ambao kweli ni wanajishughulisha na kilimo na kufahamu marejesho yao yakoje.

 Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika Bw. Godfrey Ng’urah, amesema Vijan a wanaopatiwa mkopo huo wanawakilisha vijana wengi wanaozalisha fedha katika mnyororo wa thamani wa kilimo biashara hivyo wanahitaji kuongezewa nguvu ili waweze kufikia masoko.

Benki ya Ushirika (COOP Bank of Tanzania) kwa kushirikiana na Mfuko wa Pembejeo nchini (AGITF), wametoa mkopo wa shilingi Bilioni 8.5 kwa vijana wanaojishughulisha na kilimo hususan wale walio kwenye mpango wa jenga kesho iliyo bora 'Building Better Tomorrow' ( BBT) ili vijana hao waweze kufikia malengo yao kupitia sekta hiyo.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.