• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VYAMA VYA USHIRIKA VYAPONGEZWA KWA KUHAMIA KWENYE MATUMIZI YA TEHAMA

Imetumwa : August 6th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Vyama vya Ushirika nchini vimepongezwa kwa kuondokana na matumizi ya analojia na kuingia kwenye matumizi ya Kidijitali (TEHAMA) ambayo yatawezesha wana Ushirika kuwa sehemu ya usimamizi wa Ushirika wao kwa kupata taarifa kwa wakati bila kusubiri Mkutano mkuu.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Agosti 06, 2025, katika mazungumzo mafupi baada ya kutembelea vikudi vya kuweka na kukopa (SACCOS) vilivyopo chini ya Vyama vya Ushirika katika Kijiji cha Ushirika kilichopo kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2025 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Nzuguni Jijini hapa.

“Kikubwa kilichonifurahisha wanaongea kuhusu kutoka kwenye kutumia Teknolojia ya kawaida na kwenda kutumia teknolojia ya Tehama au Kidijitali. Hicho kitu kimenifurahisha sana kwa sababu kitawezesha wanaushirika pia kuwa ni sehemu ya usimamizi wa Ushirika wao kwa sababu watakua wanapata taarifa kwa haraka bila kungoja Mkutano Mkuu.”

Pia amefurahishwa kuanzishwa kwa kitengo cha ukaguzi wa ndani wa Hesabu za Ushirika ambacho kitasaidia utunzaji wa taarifa za kifedha na nyinginezo ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa Ushirika, Wananchama na Wadau wengine wa Ushirika.

Mhe. Senyamule amesema Ushirika ni uchumi wa nchi kwani umesaidia kupanda kwa bei ya mazao kutokana na kuacha kutumia watu wa-kati kuuza mazao na kwa sasa kila SACCOS ina bei yake ambayo ni ya Kimataifa hali inayoashiria Mkulima anafaidika moja kwa moja na bei hiyo.

Awali, Mkuu huyo wa Mkoa alitembelea SACCOS mbalimabali kama vile Shirikisho la vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Moshi Co-operative University( MoCu), Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika, Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Bumaco Insurance na Ngome Saccos.

Kaulimbiu: “Chagua Viongozi Bora Kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”


#nanenanekitaifa2025kandayakati

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.