• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WABAPTIST KUJENGA MAKAO MAKUU YAO DODOMA

Imetumwa : July 16th, 2025

Na: Sizah Kangalawe

Habari – Dodoma

Kanisa la Wabaptist Tanzania (BCT) limezindua rasmi jengo la ofisi na kufungua ujenzi wa Makao Makuu ya Kanisa hilo Jijini Dodoma, ikiwa ni maandalizi ya kuhamishia shughuli  zao za kiofisi  katika Jiji hili.

Tukio hilo limefanyika Jumatano ya Julai 16, 2026 Jijini Dodoma, katika Mkutano Mkuu wa 49 wa Kanisa hilo. Mgeni rasmi akiwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Prof. Kabudi alilipongeza kanisa hilo kwa utume wao wa kutangaza injili na kuhudumia jamii kwa miaka 69 tangu lilipoanzishwa mwaka 1956.

"Niwapongeze kwa utumishi wenu tangu mwaka 1956, maana yake mwakani mnatimiza miaka 70—ambayo ni Jubilee ya Almasi. Pia nawapongeza kwa kuwa na waumini zaidi ya milioni 2, sawa na zaidi ya asilimia 4 ya Watanzania wote.

Aidha, aliwapongeza kwa mchango wao katika kutoa huduma za kijamii na kiroho kwa wananchi.

"Nawapongeza kwa kazi kubwa mnayofanya —pamoja na huduma za kiroho, mmekuwa mkihudumia jamii kwa kuanzisha vyuo vya thiolojia, shule, zahanati na vituo vya afya. Mmeendeleza maisha ya watu kiakili, kimwili na kiroho. Hongereni sana", aliongeza Prof. Kabudi.

Vilevile, alieleza kuwa Mhe.  Rais Dkt. Samia ameahidi kuchangia shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Anorld Manase Mollel, alitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa ushirikiano mkubwa ambao serikali imetoa.

"Kipekee namshukuru Mkuu wa Mkoa. Umekuwa msaada mkubwa kwetu, hasa kwa kuwa kiwanja hiki kilikuwa kikitamaniwa na wengi. Wakati tunakinunua, kilikuwa kikubwa mno na Serikali haikuwa imehamia Dodoma. Baada ya Serikali kuhamia, changamoto ziliongezeka, lakini kupitia ushirikiano na ofisi ya ardhi, tumefanikisha ujenzi huu", alisema Askofu Mollel.

Akitoa salamu za mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, aliahidi kuendelea kushirikiana na Kanisa hilo kwa karibu.

"Nimpongeze Askofu ambaye leo amekuwa rasmi Askofu wa Kanda ya Kati. Tumekuwa tukishirikiana naye kwenye mambo mengi. Kwa heshima hiyo kubwa aliyokabidhiwa na Mungu, hongera sana.

"Niendelee kukuahidi, Askofu Elyashimba, kuwa tutatoa ushirikiano ili kuhakikisha kanisa linaendelea kuwa na amani, utulivu, na kustawi. Serikali ipo tayari wakati wowote mtakapohitaji msaada wetu", aliongeza Mhe. Senyamule

Awali, akisoma risala kwa mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Kanisa hilo alisema kuwa ujenzi wa Makao Makuu hayo unakadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 800, ambapo hatua mbalimbali za ujenzi zinaendelea.

Kanisa la Wabaptist Tanzania (BCT) lilianzishwa mwaka 1956 na kusajiliwa rasmi mwaka 1971. Hadi sasa, limeenea nchi nzima, likiwa na jumla ya kanda 7, majimbo 57 na waumini zaidi ya milioni 2.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WABAPTIST KUJENGA MAKAO MAKUU YAO DODOMA

    July 16, 2025
  • WANAWAKE WAOMBOLEZAO KUKUTANISHWA KWENYE KONGAMANO KULIOMBEA TAIFA DODOMA

    July 16, 2025
  • SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA WAFANYABIASHARA WANAKUWA NA MAZINGIRA RAFIKI

    July 14, 2025
  • MZUMBE MBIONI KUANZA KAMPASI DODOMA

    July 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.