• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAFANYAKAZI MSISAHAU JUKUMU LA MSINGI LA MALEZI-SAGINI

Imetumwa : May 1st, 2023


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Mhe.Jumanne Sagini ametoa wito kwa Wafanyakazi wote, mbali na kazi zao za msingi za kila siku wanazozifanya kutosahau kuungana kwa pamoja katika malezi ya watoto na kusimamia maadili mazuri ili kutengeneza kizazi kizuri kwa ujenzi wa taifa.

Mhe.Sagini ametoa Wito huo leo Mei 1,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza Katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.  

"Najua tuna kazi nyingi ila tusisahau jukumu letu la msingi la malezi hili haliepukiki na tukizembea hapa tutatengeneza kizazi ambacho hakitakuja kusaidia jamii wala taifa kwa miaka ijayo," Amesema Mhe.Sagini


Pia Sagini amewataka waajiri kuhakikisha wanawasilisha michango ya waajiriwa wao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kutokufanya hivyo wanawanyima haki ya msingi waajiriwa wao na kusababisha misuguuano yanapotokea matatizo.

"Na nyie Mifuko ya jamii msikae kimya kwa waajiri ambao hawapeleki michango na msisubiri mpaka mtumishi afariki ndio muanze kufuatilia kwa sababu sio sawa shughulikieni haya mapema ili kuepuka minong'ono," amesisitiza Mhe.Sagini


 Aidha amewataka waajiri kuacha tabia ya kuwachagulia wafanyakazi vyama vya wafanyakazi vya kujiunga navyo kwani kufanya hivyo ni kuwanyima uhuru wao kwani kila mfanyakazi ana uhuru wa kuchagua ni Chama gani ajiunge nacho.


Naye, Mwenyekiti wa TUCTA Dkt Leonia msafiri ambaye alisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi Mkoa wa Dodoma ameshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha stahiki za wafanya kazi siku hadi siku.


Aidha, halfa hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiowemo viongozi wa Serikali, Wakuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Kongwa pamoja na Taasisi mbalimbali za umma.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.