• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAFANYAKAZI WA TANESCO WATAKIWA KUWA MABALOZI WA MATUMIZI YA NISHATI YA UMEME KUPIKIA

Imetumwa : August 14th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), wametakiwa kuwa Mabalozi wa Ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kutokana na tafiti kuonesha kuwa ‘Majiko janja’ ya umeme yanaweza kutumia chini ya unit 1 ya umeme ambayo ni sawa na shilingi 352 kuandaa mlo mmoja.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri mwenye dhamana ya Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, amebainisha hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya utoaji majiko ya umeme kwa bei ya ruzuku kwa Wafanyakazi wa Shirika hilo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Agosti 14, 2025.

Mhe. Dkt. Biteko ameongeza kuwa, ili kusukuma Ajenda ya nishati safi, Wafanyakazi wa TANESCO lazima wawe wa kwanza kutumia nishati hiyo na si kuhubiri tu maana takwimu za 2022 zinaonesha Watanzania wanaotumia nishati hiyo kupikia ni 4.2% ambayo ni ndogo kwa Tanzania inayotumia umeme hivi sasa.

“Kwa historia na mazoea tuliyonayo, watu huamini kuwa kutumia nishati ya umeme kwenye kupika ni ghali sana na hivyo huikwepa nishati hiyo kwa hofu hiyo tu. Tafiti zimeonesha kuwa, Majiko janja ya umeme yanaweza kutumia chini ya unit 1 ya umeme ambayo ni sawa na shilingi 352 kuandaa mlo mmoja”.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Lazaro Twange, amesema Mpango huo unalenga kutimiza matakwa ya Serikali kufikia 2034, asilimia 80 ya Kaya ziwe zimehama kutoka kwenye matumizi ya nishati chafu kupikia na kuhamia nishati safi ambapo wao kama wazalishaji wa umeme kwa sasa wamefikia 4% ya matumizi ya nishati hiyo kupikia.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, shilingi Bilioni 214.3 zimetolewa kwa Mkoa wake ambazo zimekamilisha usambazaji wa umeme katika Vijiji 580 vya Mkoa huu sambamba na kusambaza nishati hiyo kwenye migodi, visima vya maji na vituo vya afya.

Mpango wa utoaji wa majiko ya umeme kwa wafanyakazi hao, umeanza kwa kutoa majiko 11,000 ambayo yametolewa kwa ruzuku kwani Mfanyakazi atalipia gharama nafuu baada ya kupatiwa jiko hilo na kutakiwa kwenda kulitumia ili kuthibitisha unafuu wa matumizi ya nishati ya umeme kupikia na kuwa mfano kwa jamii ambayo ndio wateja wao.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • ASASI ZA KIRAIA ZAPEWA MAFUNZO YA KUZUIA UTAKATISHAJI FEDHA HARAMU NA VITENDO VYA KIGAIDI

    August 14, 2025
  • WAFANYAKAZI WA TANESCO WATAKIWA KUWA MABALOZI WA MATUMIZI YA NISHATI YA UMEME KUPIKIA

    August 14, 2025
  • WAFUGAJI WAASWA KUFUGA KWA KUZINGATIA UWEZO WA MALISHO ILI KUPATA TIJA

    August 13, 2025
  • MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI NI CHACHU YA MAENDELEO KWA WANANCHI

    August 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.